Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kumpa dhamana Mwandishi wa Habari Dinna Maningo wa mkoani Mara na mwenzake Costantino Mathias wa mkoani Simiyu wanaoshikiliwa na kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya saa 24 bila kudhaminiwa wala kufikishwa mahakamani.
Waandishi hao wa habari wanaoshikiliwa na Polisi wakihusishwa na uvujishaji wa siri za upelelezi wa Polisi kwenye uchunguzi wa tuhuma za aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Yahya Nawanda kudaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wa chuo mkoani Mwanza.
Wanahabari hao katika kutekeleza majukumu yao ya kufichua uhalifu na uovu unapotendeka au kupangwa waliarifu tukio hilo kwa umma hivyo Polisi inahusisha pamoja na wengine kadhaa kuripoti tukio hilo kana kwamba ni kosa wakati ni wajibu wao.
Katika kuelezea hilo, Wakili Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi ambaye ni mpigania haki za binadamu amekemea kushikiliwa wanahabari hao akisema wamakamatwa kinyume cha sheria hivyo kuitaka polisi kujitafakari na kwamba watashtakiwa kwa kushindwa kuheshimu haki za wananchi.
Mwabukusi ameitaka Polisi kuwaachia kwa dhamana waandishi habari hao kama ilivyofanyiwa kwa mtuhumiwa (Dkt.Yahya Nawanda) ambaye alishadhaminiwa huku mwandishi Dinna akikaa mahabusu kwa zaidi ya siku nne.
0 Comments