Header Ads Widget

WAASWA KUFANYA MAZOEZI KUEPUKANA NA MAGONJWA.

 TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII



Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wametakiwa kutumia muda wa ziada kukuza vipaji walivyonavyo ili viwe msaada katika maisha yao.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Gidlove Mbwaji, alipokuwa akihitimisha wiki ya Tamasha la Michezo na Vipaji liloshirikisha watumishi wa Hospitali hiyo.


"Tumepata fursa ya kuonyesha vipaji vyetu, tuviendeleze hivyo vipaji vitufikishe mbali kama wewe ni mwimbaji, mchekeshaji, naomba  tufanye katika muda wa ziada na vitufanikishe zaidi katika maisha yetu", amesema Dkt. Dkt. Godlove Mbwanji.


Aidha Dkt. Mbwanji ameitaka jamii pia kuwa na tabia ya kutenga muda wa ziada kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza.



"Nitoe wito kwa jamii kwamba ni muhimu sana wafahamu mtaji mkubwa katika maisha yao ni afya yao, ni vizuri utumie muda unaopata kufanya mazoezi na mazoezi yawe sehemu katika maisha yao”, amesisitiza Dkt. Mbwanji.


Dkt. Uwesu Mchepange ni mwenyekiti wa kamati ya tamasha la Michezo na Vipaji MZRH, amesema lengo la tamasha hilo kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ni kuwaleta watumishi pamoja na kuibua vipaji mbalimbali walivyonavyo.


“Tuliona pia tuwe na tamasha maalumu kwa ajili ya watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa lengo la kuwakutanisha waweze kuonyesha vipaji mbalimbali katika maeneo mbalimbali”, amesema Dkt. Uwesu Mchepange.


Kwa upande wao washiriki wa tamasha hilo la michezo na vipaji MZRH wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya chini ya Dkt. Godlove Mbwanji, kwa kuwa imekuwa sehemu ya burudani pamoja na kuwaimarisha kiafya na hivyo kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.


Tamasha hilo  limefanyika kwa muda wa wiki moja chini ya udhamini wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya  likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta Kamba, maonyesho ya mavazi, maigizo, mpira wa pete, mpira wa wavu, ambapo washindi wamekabidhiwa zawadi ya pesa taslimu pamoja na vikombe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI