SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA
KUANZA KUTUMIKA MWAKA MPYA WA FEDHA .
NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA APP DODOMA
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira ,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patribas Katambi amewataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa umma wa kielektroniki ujulikanao kama NeST ili kuondoa urasimu na kukuza uwazi.
Akizungumza kwenye semina ya Wabunge hao iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma alisema mfumo huo ni tiba na imara kwani utasaidia kuleta maendeleo kiuchumi na kupiga Vita ufisadi.
Alisema kuwa Mfumo huo utafanya utendaji kazi kuongezeka kwa kiasi kikibwa cha usawa na ushidani kuongezeka zaidi pamoja na uwazi katika utendaji kazi.
Pia alisema Mfumo utasaidia ufuatiliaji ambapo mfumo wa kuripoti hautakuwa mgumu tena kama jinsi ambavyo ingelazimika kwenda kuchambua makaratasi ya hapa na pale na hata data kwa jamii ,wataalamu na wabunge wanauwezo wa kupata kwa wepesi zaidi kwani data zitakuwa kwenye mfumo.
"Kuta kuwepo kwa uzingatiwaji wa viwango hasa kwenye maeneo ya kanuni kama hazijazingatiwa mfumo utakuonyesha kama kunahaki ya kukata rufaa mfumo utaonyesha,"alisema.
Aliongeza kuwa" Mfumo utasaidia kuongeza Viwango vya kimataifa vinavyotaka mifumo ya manunuzi kufuatwa na kuzingatiwa kwa kiwango kwani kila kitu kitafanyika kwenye mifumo ambapo uwazi wa kiasi cha juu utaonekana,"alifafanua.
Kadhalika alisema kuwa mfumo huo utaboresha mahusiano bora ya wasabazaji au wadau wenyewe kwenye mfumo mzima kwa kuwa na mahusiano bora kwani Mambo yataonekana kwenye mfumo na itaondoa urasimu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Eliakimu Maswi alisema Sheria Mpya ya Namba 410 ya Ununuzi wa Umma itaanza kutumika tarehe 17 mwezi Juni huku Kanununi kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu 2024
Akifafanua zaidi kuhusu mfumo huo, Maswi alisema mpaka sasa umeshaunganishwa na mifumo 18 ya serikali ikiwemo TARI, CRB, TCRA, OSHA, WCF, BRELA, NSSF na nyinginezo huku akitumia nafasi hiyo kuziomba taasisi nyinginezo za serikali ambazo bado hazijajiunga na mfumo huo kufanya hivyo.
Alisema mfumo huo wa NeST unaendana na mahitaji mapya ya teknolojia pamoja na maelekezo ya Serikali ya kuimarisha eneo la ununuzi, PPRA ilianza zoezi la kusanifu mfumo huo kwa kuzingatia misingi mikuu ya kimataifa ya ununuzi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga alieleza kuhusu mfumo wa NeST kwa nini wamefanikiwa na faida walizozipata kwanza walianza kutoa elimu Kati ya wadau wa ununuzi na watumishi wa serikali .
Lakini pia alisema walienda kutoa elimu kwa ofisi za chama cha mapinzi CCM ambapo mwenyekiti na katibu wa chama walipewa elimu ili na wao wawe mabarozi na kutoa ushirikiano.
"Baada ya kutoa elimu tukaanza kutumia mfumo kwa kutenga chumba kimoja na kuweka kompyuta 3 kwaajili kusaidia pale patakapokuwa na shida,"alisema Msanga.
Mwisho.
🛑karibu utangaze na Matukio Daima media ☎️0673791054/0747044508
0 Comments