Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp
Kamisaa wa Sensa Tanzania Anne Makinda amesema vijana nchini Tanzania wanatakiwa wafundishwe kuwa nchi hiyo ni yao hivyo kupitia dira 2050 inayofanywa waseme wanataka nchi yao iweje.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam walipokua katika kikao cha kubadilisha mawazo na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNFPA, NBS pamoja na Ubalozi wa Uengereza ambapo wamekutana kujadili namna ya kuzichataka taarifa za sensa kwa ajili kuzisambaza na kuzitumia.
Amesema kuwa, tangu mwanzo wa mchakato wa sensa wamekua pamoja hivyo sasa umefika wakati wa kuzichataka lazima ushirikiano wao uendelee kwa ajili ya kupata taarifa sahihi na kuzitumia katika sehemu mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
"Tulianza kuwahamasisha watu wajiandikishe, tukaingia hatua ya pili ya sensa ambapo wameshiriki na sasa tupo sehemu ya tatu ya kuzichakata na kuziweka katika sura ambayo inakubalika kitaifa na kimataifa"amesema Kamisaa Makinda.
Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo cha idadi ya watu kutoka UNFPA Samweli Elisa Msokwa amesema kuwa UNFPA ina wajibu wa kuunganisha wadau wa maendeleo katika kufanya kazi na Serikali kwenye maendeleo ya takwimu hasa kwenye sensa ya idadi ya watu.
Amesema kuwa, Unfpa imeisaidia Serikali katika kuleta maendeleo ya pamoja katika hatua ya kwanza kutenga maeneo ya pili kuhesabu na sasa wapo hatua ya tatu ya kuchakata kwa ajili ya maendeleo mbalimbali na kuweza kuzisambaza kwa ajili ya matumizi.
"Leo tulikua na ubalozi wa Uengereza ambapo tulijadili maeneo matano tunasaidiana na Serikali kwenye maeneo ya afya, uhamiaji, elimu, na takwimu za watu, katika mjadala huu tumekubaliana kupeleka wataalamu wetu kwenye hizi takwimu ambalo taifa limekua likiendelea nalo pamoja na dira 2050.
"kwenye huu mchakato tutatumia wataalam wetu wa ndani kwani wana uwezo mkubwa hii ni sensa ya 6 Tanzania imejijengea uwezo hivyo takwimu hizi zitatumika kuanzia nchini hadi Taifa"amesema
Naye, Gertude Mapunda Kutoka ubalozi wa Uengereza amesema kuwa kupitia sensa wamekua wakitoa msaada kupitia UNFPA ambao wamekua kiunganishi chao na Serikali ya Tanzania .
"Tulianza kukusanya data, kuhesabu na sasa wanazichakata kwa ajili ya matumizi taarifa hizi zinatakiwa zisambazwe ili wadau mbalimbali waweze kuzitumia"amesema Mapunda
0 Comments