Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga Juni 07, 2024 alipotembelea Kata ya Itumpi Wilayani Mbozi kwa lengo la kutoa elimu ya umuhimu wa ulinzi jirani na madhara ya uhalifu na wahalifu katika jamii.
Kamanda Senga amenukuliwa akisema kuwa
"Kila mwananchi akichukia vitendo vya kihalifu na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika suala la ulinzi wa mali zetu ni dhahiri jamii yetu itakuwa salama kwa ustawi wa kila familia na jamii kwa ujumla", amesema Kamanda Senga.
Aidha Senga amewataka wananchi hao kushirikiana na viongozi wa maeneo yao kukemea vitendo viovu katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wageni wanaofika katika katika jamii zinazowazungukana kwani baadhi wawekuwa wakiwapokea watu na baadaye kufanya vitendo vya kihalifu na kutokomea bila kuwa na taarifa zao.
0 Comments