Header Ads Widget

MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA YAFIKIA ASILIMIA 5 KUTOKA 7

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

MAAMBUKIZI ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kutoka asilimia 7 hadi kufikia asilimia 5 ambapo lengo ni kufika chini ya asilimia 4 . 



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela ameeleza hayo leo June 7,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wake na vyombo vya habari kuhusu hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa vijana wa kike. 


Amesema walianza mabali katika kuhakikisha wanatokomeza  maambukizi hayo ambapo Kama Tume matarajio yao pendwa ni kufikia asilimia 4 hali itakayoonesha wamefanikiwa kuondoa au kutokomeza maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto. 


 "Tunaimani kwa juhudi zinazofanyika na Serikali kupitia Tume tutafikia malengo kwasababu kama katika jamii kiwango cha kufubaza kipo asilimia 1 chini ya lengo la kidunia ambapo humo kwenye asilimia 1 wapo wa mama wajawazito na wengine, " 


Na kuongeza "Hivyo hatuna shaka kwamba katika muda mfupi tutakuwa fikia kiwango cha chini ya asilimia 4 ambapo tutakuwa tumeweza kutokomeza kabisa maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto, " Amesema


Aidha amesema Idadi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini imeendelea kupungua kutoka watu 72,000 mwaka 2016/2017 hadi kufikia watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023 idadi ambayo sawa na punguzo la asilimia 16.


"Ingawa kiwango cha maambukizi mapya kimeelendelea kupungua kwa makundi yote, kiwango cha maambukizi mapya ya Virusi hivyo kwa kundi la vijana wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24 kimeongezeka kutoka asilimia 0.14 kwa mwaka 2016/2017 hadi asilimia 0.33 kwa mwaka 2022/2023, " Amesema


Hata hivyo ametaja visababishi vya kupanda kwa maambukizi hayo kwa wasichana kuwa ni pamoja na kutokuwa na uelewa wa kutosha wa mbinu za kujikinga na maambukizi mapya, ndoa za utotoni, kufanya ngono zembe, utandawazi, tamaa, umaskini na kujihusisha na wapenzi zaidi ya mmoja. 


Ameeleza kuwa utafiti wa viashiria vya VVU na Ukimwi mwaka 2022/2023 kiwango cha ushamiri wa VVU kitaifa ni asilimia 4.4 ambapo kwa wanawake ni asilimia 5.6 na wanaume asilimia 3.0.


"Hii inamaanisha kwamba jumla ya watanzania 1,548,000 wanaishi na maambukizi  ya VVU , umri wenye kiwango kikubwa cha ushamiri kwa wanaume ni miaka 50-54 kwa wanawake ni miaka 45 hadi, " ameleeza


Dkt. Kamwela ameeleza kuwa TACAIDS kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutekeleza afua mbalimbali zinazowalenga vijana wa umri wa miaka 15-24 waliopo shuleni na wale walio nje ya shule ili kuwapatia elimu ya stadi za maisha kuondokana na ushawishi utaopelekea kupata maambukizi. 


"Afua hizo ni pamoja na zile zilizoyekelezwa kwa kuwahisisha vijana balehe na wanawake (AGYW)kupitia mradi wa Timiza malengo wa DREAMS ili kuwapatia elimu ya VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na stadi za maisha, wasichana walio nje ya shule wakewezeshwa kiuchumi na kuwa salama , "ameeleza 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI