Header Ads Widget

HALMSHAURI ZINUNUE MAFUTA KINGA KWAAJILI YA WENYE UALBINO NCHINI - NDEJEMBI



WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye ulemavu Deogratius Ndejembi amezitaka Halmashauri Nchini kutenga bajeti ya fedha Kwaajili ya  kununua Mafuta kinga dhidi  ya mionzi ya jua kwa Watu Wenye Ualbino kwakuwa jukumu la Halmashauri za wilaya nchini ni kuhudumia  Wananchi.


Ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya kuongeza uelewa juu ya ualbino IAAD duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mailmoja wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo Waziri Ndejembi amewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema hayo ni maagizo ya serikali kwa halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga bajeti ya fedha kwaajili ya kununua mafuta kinga dhidi ya mionzi ya jua kwa watu wenye vilemea vya ualbino.



Amesema “Halmashuari zote zihakikishe zinatenga bajeti na fedha zinapatikana na fedha hizo zinanunua  mafuta yenye kutoa kinga dhidi ya mionzi ya jua maana mnaweza kusema mmeweka kwenye bajeti lakini changamoto ni kwamba bajeti hiyo fedha haipatikani au fedha zikipatikana hazifanyi kazi ya kununua mafuta hayo”


“Hivyo tunaagiza fedha hizo ziwekwe kwenye bajti na zipatikane na mnunue mafuta hayo kama ambavyo mnafanya kwenye huduma zingine na mfahamu hili ni la muhimu zaidi kwani linahusiana na uhai wa maisha ya wanadamu wenzetu” amesema Ndejembi. 



Aidha kizungumzia ushiriki wa chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kwa kusema “watu wenye ualbino mnahaki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi hivyo muitumie vizuri nafasi hiyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani”  


Hata hivyo amesema serikali inaelekeza maafia Elimu maalumu na maafisa ustawi wa Jamii waa mikoa na halmashauri nchini kuhakikisha wanafanya utambuzi wa watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino na Kufanya usajili wa Watu hao wenye Ualbino rejesta ya kumbukumbu za watu wenye ulemavu katika ofisi za watendaji wa mitaa na vijiji na huisha kila nusu mwaka kama taratibu zinavyoelekeza. 

 


Awali Mwenyekiti  wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino (TASS) Godson Mollel ameiomba serikali  kuwawekea nazingira ya usalama watu  wenye Ulemavu  wa Ngozi Ualbino nchini  katika kuelekea  kipindi cha  Uchaguzi  wa Serikali za mitaa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu  na Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2025.



Mollel amesema kipindi hili kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani kundi hilo lihakikishiwe Ulinzi na usalama wao kwani kipindi hicho huwa na Matukio pengine ya hatari kwa kundi hilo la walemavu.


Naye Raphael Meella ambaye ni Mwakirishi wa Mkuu wa jeshi la Polisi IGP Camilius Wambura amesema jeshi la Polisi nchini limejipanga kusimamia na kulinda watu hao wenye ualbino nchini ambapo tayari mapolisi kata 3945 na wakaguzi, makamishina wakusimamia Polisi jamii ili kuhakikisha usalama wao.



Hivyo amewataka kuendelea kufanya majukumu yao kwani jeshi la Polisi lipo nyuma yao kwa kutumia njia za kiusalama za kiinteligensia kuhakikisha wapo salama.


Mkurugenzi kitengo Cha huduma Kwa Watu Wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana ajira na Watu Wenye ulemavu Rasheed Mafta amesema wataendelea kushirikiana nao Katika Jamii.



Maadhimisho hayo yanefanyika kitaifa Mkoani Pwani ambapo yamefanyila Kwa siku tatu ambapo 13 June ndio kilele.

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI