Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Ramadhan Ng'anzi amewataka waendesha bodaboda kubadilika kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Usalama barabarani ili kuzuwia ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda.
Akizungumza na waendesha bodaboda wa Kituo cha Michenzani Tobo la Pili Mjini Zanzibar amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Aidha DCP. Ng'azi amewapongeza Waendesha Bodaboda wa Kituo cha Tobo la Pili kwa kuwa mfano mzuri wa kutii sheria za usalama barabarani na amewaahidi kuwa Jeshi la Polisi litakuwa karibu nao kuendeleza sekta hiyo muhimu ya usafirishaji.
Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya waendesha bodaboda Zanzibar Hussein Omar Hussein amewashukuru Viongozi wa Jeshi la Polisi kwa kuwa nao karibu na kuwasaidia kutatua changamoto zao.
0 Comments