Header Ads Widget

MAGOTI ALA KIAPO CHA UKUU WA WILAYA KISARAWE

MKUU mpya wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ameahidi kusikiliza kero za wananchi kwa kuzingatia sheria taratibu na katiba ya nchi.


Magoti ametoa ahadi hiyo Mjini Kibaha wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge.


Magoti ambaye ameteuliwa  hivi karibuni na  Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameahidi kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa weledi na uadilifu mkubwa kwa kushirikiana na viongozi wenzake.


Amesema kuwa deni alilonalo ni la kuwatumikia wananchi ili kuwaletea wananchi


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alimtaka mkuu huyo mpya kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuzingatia katiba ya nchi pamoja na kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.


Kunenge alimkabidhi vitendea kazi mbalimbali ikiwemo katiba ya nchi na ilani ya chama kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI