Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa pikipiki katika maeneo ya mikusanyiko ya watu ikiwemo kwenye harusi, misiba na nyumba za ibada.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP DANIEL SHILLAH amewataja watuhumiwa hao ni Iddi Abdalla Kisumba Miamkq 20 na Rashid Abdalla Sadala Miaka 19 wakaazi wa Kidimni, Fakih Kassim Khamis Miaka 19 mkaazi wa Amani na Ahmed Amour Abdalla Miaka 24 Mkaazi wa Makunduchi, ambao wamekamatwa katika maeneo tofauti wakiwa wameshaiba pikipiki tatu.
Aidha Kamanda shillah amesema wamefanikiwa kuwakamata watu wengine watatu ambao wanajihusisha na unyanganyi wa kutumia silaha kwa kuwavizia watembea kwa miguu huwatishia kwa mapanga na kuwapora kisha kukimbia kwa kutumia pikipiki, akiwemo Khalid Salum Said M. 20 Mkaazi wa Fuoni, Yassir Abdalla Shaaban M 30 Mkaazi wa Fuoni na Ali Mohamed Ali (Shetani Kiro) M. 28 Mkaazi wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja
0 Comments