Na Gift Mongi, Matukio daima app Moshi,
Familia moja iliyopoteza watu wanne baada ya kuangukiwa na nyumba iliyosababishwa na mvua iliyonyesha April 25 imeahidiwa kupewa kiasi cha shilingi milion tano na mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi.
Uharibifu mkubwa ukitokana na mvua hizo ikiwemo wa vyakula mifugo na pia nyumba ladhaa kubomoka na kuacha familia zikiwa hazina makazi sanjari na mali nyingine kupotea au kuharibika vibaya.
Akiwa katika ibada ya mazishi ya watu hao yaliyofanyika katika kata ya Kimochi jimbo la Moshi Vijijini Prof Ndakidemi alitoa ahadi hiyo lengo likiwa ni kuwapa faraja wafiwa lakini kuweza kujikimu.
"Kiasi hiki kinaenda kuleta faraja kama ubani lakini kurejesha makazi baada yao kuanguka hivyo kuongeza ugumu wa maisha"anasema
Prof Ndakidemi pia alitoa tani mbili za mahidi kwa wananchi wa kata za Mabogini na Arusha chini ambazo ziliathiriwa na mafuriko hayo.
Zaidi ya watu 4,000 wameripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyosabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Hata hivyo kaya 906 zimeathiriwa na mafuriko hayo huku watu sita wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.
Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Zephania Sumaye April 29,2024 Mjini Mosh wakati akipokea Misaada ya kijamii kutoka kwa msamalia mmoja kwa ajili ya wahanga wa mafuriko hayo waliopatiwa hifadhi kwenye shule ya Sekondari ya kutwa ya Lucy Lameck.
Akipokea misaada hiyo Sumaye alisema wahanga hao wa mafuriko wana uhaba mkubwa wa chakula ,huku wengi wakiwa hawana malazi huku akimpongeza msamalia huyo kwa moyo wake wa kujitolea kwa kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko ikiwemo Magodoro, Unga , Mafuta, Mchele, Sabuni, Taulo za kike , Kalamu, Madaftari pamoja na Mikungu ya ndizi.
0 Comments