Header Ads Widget

WAZIRI ULEGA AWAPA MSAADA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO MKURANGA

  WAZIRI ABDALLAH ULEGA AKIONGEA NA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Na Thobias Mwanakatwe


MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewatembelea na kuwafariji wananchi waliothiriwa na mafuriko katika Kata za Kisiju na Shungubweni, Wilayani Mkuranga, mkoani Pwani. 


Akitoa salamu za pole Mei 1, 2024, Ulega amesema kuwa Rais Samia amemtuma kuwafikishia wananchi hao salamu zake za pole pamoja na chakula, magodoro na vifaa vingine vya ndani ili viwasaidie katika kipindi hiki wakati serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi hao wanarejea katika maisha yao ya kawaida.

 WAZIRI ULEGA AKIWASIKILIZA WANANCHI

Sehemu kubwa ya wananchi hao ambao Mhe. Ulega amewatembelea nyumba zao zimeathiriwa kwa kuzingirwa na maji na kupelekea kukosa makazi na hivyo kulazimika kukaa katika makambi.

 WAZIRI ULEGA AKIKABIDHI MISAADA

Jumla ya vitu ambavyo Mbunge huyo amekabidhi kwa niaba ya Rais Samia ni Mchele tani 4, Unga tani 5 na Maharagwe tani 10 ambavyo amekabidhi kwa Vijiji vya Kerekese,Kalole,Mavunja na Kisiju pwani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS