Header Ads Widget

WANAUME NJOMBE WATUPIWA LAWAMA KUCHAGIZA UDUMAVU KWA WATOTO

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wanaume mkoani Njombe wameendelea kutupiwa lawama kuwa chanzo cha udumavu kwa watoto kwa kushindwa kushiriki kikamilifu katika malezi,Makuzi na matunzo ya watoto.


Katika kampeni ya Afya na Lishe mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe baadhi ya wanawake hao akiwemo Emmakulata Kyando na Angela Mwangeni Diwani viti maalumu tarafa ya Njombe mjini wamesema baadhi ya  akina baba Kuna wakati wamekuwa wakishindwa  kutimiza wajibu wao katika matunzo ya watoto.






Diwani wa kata ya Ramadhani Nickson Nganyange Amewataka wanaume kuelekeza fedha zao katika malezi ya Watoto badala ya kutumia kwenye starehe.


Damiana Danda ni Ofisa Lishe wa Halmashauri ya mji wa Njombe ambaye anakiri kuwapo kwa changamoto kwa baadhi ya Akina baba ambao wamekuwa kikwazo katika mapambano dhidi ya udumavu.


Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya wanaume akiwemo  Godwin Sanga,Festo Mgeni na Furaha Mwatumbwe kujua sababu za tuhuma hizo kuelekezwa kwao ambao wanasema uchumi na wanawake wenye kuwa na mambo mengi ni miongoni mwa sababu kubwa.


Walimu nao akiwemo Dorcas Nziku wanakiri kuwapo kwa ugumu wa ufundishaji watoto waliokumbwa na changamoto ya udumavu.


Halmashauri ya mji wa Njombe imeendelea na kampeni ya Lishe mtaa kwa mtaa baada ya mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka kuzindua kampeni hiyo inayokwenda kwa Kauli mbiu ya ''kujaza tumbo sio Lishe Jali unachomlisha"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI