MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini, Mhe. Pauline Philip Gekul ameibu shangwe, nderemo na vifijo, baada ya kusimama na kugusia kidogo juu ya sakata la kesi yake.
Akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi, katika bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mbunge huyo mpole na mtumishi wa Mungu, ameeleza namna ambavyo 'alikinywea kikombe' katika wakati huo mgumu, na kwamba haikuwa rahisi.
"Nimshukuru Mungu kwa namna ambavyo amekuwa akitubariki sote, Kila moja wetu kwa namna yake, hata pale tunapopitia magumu, yeye hutusaiia kwa namna ya kipekee," alisema na kuongeza;
"Hata mimi, katika kipindi kigumu nilichopitia, haikuwa rahisi kwamba leo nimeweza kusimama hapa, lakini kwa maombi ya Watanzani na kudra zake Mungu, leo nasimama kwa ujasiri kuendelea na majukumu yangu ya kibunge.
"Nimevipisha vyombo vya Sheria kuendelea na kazi yake, lakini ukweli utabainika, tujijengee Utamaduni wa kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa.
"Pia nimshukuru sana Rais, Dkt. Samia kwa namna ambavyo ameniamini mimi binti yake, amenitoa mbali, ni mama msikivu, mwenye huruma na mzalendo wa kweli, Mungu akubariki Mhe. Rais na sisi wana Banati hatuna deni na wewe," alisema Mhe. Gekul kwa sauti ya ujasiri na busara thabiti.
0 Comments