Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri wa katiba na sheria Balozi Dokta Pindi Chana amesema zaidi ya Migogoro 500 imeshughulikiwa kupitia kampeni maalumu ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid pasina gharama yoyote inayoendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa safari hii mkoa wa Njombe utakwenda kufikiwa.
Mbele ya vyombo vya habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Dokta Pindi amesema mikoa 6 imefikiwa na timu ya mawakili hao kwa kuwafikia wananchi laki 415000 elfu ikiwa katika mkoa wa Njombe kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mei 26 mwaka huu katika Kituo cha mabasi cha zamani Mjini Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema Vijiji 180 vilivyopo kwenye kata 60 mkoani hapa vitafikiwa na huduma hiyo itakayokwenda kwa siku 10.
Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo France Msanga mwenyekiti wa mtaa wa Kambarage na Lilian Lugome ambao wamesema kampeni hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwani Njombe kumekuwa na wimbi kubwa la ukatili wa kijinsia,migogoro ya ndoa,Ardhi pamoja na mauaji.
Given Mtweve ni mwenyekiti wa Shujaa wa maendeleo na kupinga ukatili mkoa wa Njombe ambaye anakiri kuwapo kwa vitendo vya ukatili ambavyo vinapaswa kutokomezwa.
Kampeni ya Mama Samia Legal Aid huenda ikawa muarobaini wa kupunguza kero ambazo wananchi wamekuwa nazo kwa muda mrefu kwa kukosa fedha za kuwatafuta mawakili.
0 Comments