WANAWAKE na vijana wametakiwa kujitokeza kushiriki katika kongamano la Biashara linalotarajiwa kufanyika Mei 28 hadi 31 mwaka huu
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Tabwa na mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake wafanyabiashara Kimataifa Noreen Mawalla amesema kuelekea maadhimisho ya siku ya Afrika wameandaa kongamano la Biashara pamoja na maonyesho ya biashara ya kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salama Mawala amesema kongamano hilo ambalo ni la tatu litahusisha wajasiriamali, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa maendeleo
Mkurugenzi huyo amesema lengo kubwa ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya manufaa ya kufanya biashara katika eneo la soko huru la Afrika.
"Kama mnavyofahamu Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimerudhia katika eneo la soko huru la Afrika, na ziko takeibani nchi 54 lengo lake ni kuwa na soko la pamoja katika Bara Zima la Afrika, kwa mara ya tatu tunaandaa kongamano hili kutoa elimu na watu kujua fursa zinazopatikana katika eneo la soko huru la Afrika,"amesema
Mawala amesema soko hilo ambalo ni kubwa kuliko masomo yote linatarajiwa kuwa na wateja Bilion 1.3 katika bara zima la Afrika na kupitia kongamano hilo wataongelea itifaki ya Wanawake na vijana katika fursa eneo kuu la soko huru la Afrika.
"Pia wako Wanawake ambao wamekuthubutu kufanya biashara katika nchi nyingine za Afrika tutawatambua, watatoa historia yao na manufaa waliyopata kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wengine waweze kuthubutu," amesema.
Mratibu wa kongamano hilo Meshack Robert amesema kongamano hilo linashirikisha mataifa ya afrika hivyo ni fursa kwa vijana Wanawake kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Meshack amesema bidhaa nyingi zinazotumika kwenye mataifa mbalimbali zinatokea Afrika, hivyo uzalishaji unatakiwa kuwa mkubwa utakaowezesha bidhaa kukuzwa maeneo mbalimbali na kukuza uchumi.
0 Comments