Header Ads Widget

KIONGOZI WA MWENGE ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI 6 YA MAENDELEO WILAYA YA KATI UNGUJA

NA Matukio Daima App- ZANZIBAR

KIONGOZI wa mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 Godfrey Eliakimu Mzava ameridhishwa na miradi 5 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 38 ambayo imepitiwa na Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa miondombinu ya Barabara, Tangi la Maji, Skuli, Nyumba za madaktari Afya, Ujenzi wa hoteli ya kitalii pamoja na upandaji wa miti.

Amesema, miradi yote ya maendeleo ndani ipo katika hatua nzuri kukamilika kwake licha uwepo wa mapungufu madogo madogo ambayo Wilaya na mkoa inabidii kuchukua hatua stahiki ili kuboresha zaidi.

"Nimeridhishwa na utekelezaji wa Miradi yote ambayo imepitiwa na mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, kimachotakiwa miradi hii iendelezwe na ikamilike kwa wakati," ameeleza.

Aidha ametoa rai kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha miradi hiyo inamaliza kwa ubora na wakati uliokusudiwa.

"Wakandarasi na wasisimazi wa miradi hakikisheni hii miradi inamaliza kwa wakati, inamaliza kwa ubora unaokidhi kiwamgo," amesema.


Mapema Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa mwenge wa uhuru kitaifa unekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo nchini kwa kufungua miradi mbalimbali.

"Mwenge wa Uhuru umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa kuzindua miradi ya maendeleo," amesema.

"Tunatakiwa kujifunza mengi sana kupitia mwenge wa uhuru kwa ujumbe ambao umebeba ambao kila mwaka umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo nchini," ameeleza.

Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa Kusini Unguja yamefanyika katika Viwanja vya Kilombero na inatarajiwa kutembelea zaidi ya Miradi 11.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI