Header Ads Widget

PWANI MGOMBEA URAIS MWAKA 2025 NI DKT SAMIA SULUHU HASSAN TU

 


TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Na Scolastica Msewa, Kibaha

KATIBU wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani David Mramba amesema mkoa huo katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 itatambua fomu moja tu ya kuomba kugombea Uongozi wa nafasi ya urais ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tu Ili aendeleze kasi ya alipoishia kwenye utekezaji wa miradi ya maendeleo nchini.


Mramba ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki alipozikutanisha mashirika 22 yasiyo ya kiserikali ambayo yanamrengo mmoja wa kukisemea chama na Serikali na kusisitiza uzalendo kwa wananchi zinazofanya kazi zake katika Mkoa wa Pwani.


Alisema katika Mkoa huo ipo miradi mingi imetekelezwa na inahitaji kuendelezwa na kukamilishwa hivyo kutokana na hali hiyo katika uchaguzi 

Mkuu fomu ya Rais kutoka chama hicho itakuwa kwa ajili mgombea mmoja pekee wa nafasi ya urais.


Alisema mwingine yeyote atakayechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo hawatamtambua ili malengo yao kimkoa na taifa yatimie, huku Viongozi na wanachama wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyokuwemo ukumbini walipiga kelele za mashangilio kuonyesha kukubali pointi hiyo.

Aidha Mramba aliwataka mashirika hayo  yanayoanzishwa kwa mrengo wa kuisemea Serikali na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt Samia Suluhu Hassan yanatakiwa kuhakikisha hayatumiki kama kichaka cha maovu.


Katibu huyo alisema yapo baadhi ya mashirika yamegeuka kichaka cha kuhifadhi maovu, kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya uanzishwaji na kuchafua Serikali na chama tawala jambo ambalo sio halipendezi kwa jamii.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI