Header Ads Widget

KISHINDO CHA BOMU BARIDI CHATUA SAME, DC AFUNGUKA KUHUSU TEMBO

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi ambazo amekuwa akizifanya kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa hasa kwa kufanya tafiti mbalimbali za kutatua changamoto ya uvamizi wa Wanyama pori waharibifu kwenye jamii ikiwemo Tembo.



Kasilda amezungumza hayo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bomu baridi ambalo litatumika kwenye maeneo yenye changamoto ya wanyama waharibifu kwa upande wa Wilaya ya Same na Mwanga.



 "Miongoni mwa changamoto ambayo tunakabiliana nayo sisi wakazi wa Same ni uvamizi wa wanyama waharibifu ikwemo Tembo ambao wamekuwa wakiharibu mazao na kuhatarisha usalama wa wananchi, lakini kwa hatua hii iliyofikiwa na Serikali imani yangu mwarobaini wa changamoto ya Tembo kwenye wilaya yetu umepatikana" Alisema Kasilda...



Aidha amempongeze Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki kwa jitihada na ubunifu mzuri wa bomu baridi pamoja na kikosi cha Mzinga Morogoro kwa kuliboresha bomu hilo kwa umahiri mkubwa.



Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Same, Amos Kusakula amepongeza hatua ya iliyochukuliwa na Serikali kwenye utatuzi wa changamoto ambayo kimsingi ilikuwa imigonga vichwa vya wakazi wengi wa Same hasa inapofika nyakati za kiangazi ambapo tembo huhangaika sana kutafuta chakula na maji.



Awali akielezea mchakato wa kupatikana kwa bomu hilo Dr. Emanuel Masenga ambaye ni daktari wa Wanyama Taasisi ya utafiti wa Wanyama pori Tanzania TAWIRI amesema Taasisi hiyo inajukumu la kufanya tafiti za kina kutafuta teknolojia bora ambayo itasaidia kudhibiti Wanyama waharibifu ikiwemo Tembo pindi wanapovamia mashamba na makazi ya watu.



Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI