Header Ads Widget

TAMASHA LA ZIFF LA 28 LAZINDULIWA KWA MATEMBEZI YA AMANI


Na Andrew Chale, Zanzibar


TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) ambalo mwaka huu ni la msimu wa 28, limezinduliwa rasmi kwa shamra shamra za matembezi asubuhi ya leo tarehe 25-6-2025 katika viunga vya Mji Mkongwe, Unguja, Zanzibar.

Katika matembezi hayo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, ambaye ndiye mwenyeji wa Tamasha, Mhandisi Ali Said Bakar, alisisitiza umuhimu wa ZIFF kwa jamii na sanaa.

Katika hotuba hiyo iliyosomwa kwa Niaba yake na Ofisa kutoka Mamlaka hiyo, Bi. Asha Ali Hassan amesema kwamba tamasha hilo likitimiza miaka 28 limeonesha kuwa msaada mkubwa kwa jamii na katika uchumi wa Zanzibar ikiwamo kutunza utamaduni na sanaa ya filamu.

Bendi ya Polisi ikiongoza matembezi hayo 



Aidha Mhandisi Bakar alisisitiza umuhimu wa mazoezi ya kimwili na kiakili, akisema, "Hapa leo tunaungana kwa kufanya mazoezi, kwani ni moja kati ya tiba ya kimwili na akili katika ufanisi wa kazi zetu za kila siku."

Alionyesha kufurahishwa kwake na ZIFF kwa kuwakusanya wanamazoezi, wasanii, wanahabari, na wadau wote wa tamasha hilo kama familia moja ya kazi za Sanaa na uigizaji.

Pia, alisisitiza jinsi mazoezi hayo yalivyoleta faraja kwa wanajamii wa Mji Mkongwe na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji.

Pia amesisitiza haja ya kuwapatia vijana historia ya mji wao kupitia shughuli kama hizo za tamasha, na akawapongeza ZIFF kwa kuendelea kuupamba Mji Mkongwe.

Mwenyekiti wa Vikundi vya mbio Zone A, Bwana Sitwale akizungumza mara baada ya matembezi hayo

"Tamasha hili ni letu," alisema Mhandisi Bakar, akiwahimiza wananchi kutumia fursa zinazotolewa na ZIFF kudhamini juhudi zao za kuwaunganisha, kuwaelimisha, na kuwazindua mambo ambayo hawajui au wamesahau katika kujiletea maendeleo kupitia Sanaa ya Filamu.

Mhandisi Bakar aliahidi ushirikiano wa serikali na ZIFF, akisema, "Sisi Serikali tunathamini sana mchango wenu kwa Taifa letu nasema tuko pamoja katika 'TUMAINI LINAPOCHIPUKIA'."

Aliwakaribisha ZIFF katika Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, akisisitiza umuhimu wa kusaidia wasanii, hasa wa filamu, na majukwaa ya watoto na vijana, kwani wanasaidia serikali kufikia malengo yake Kitaifa na Kimataifa.

Naye Mratibu wa Jukwaa la wanawake na Vijijini la ZIFF, Bi. Sabrina Faraja amesema kwamba: "Maandamano haya ni kitu cha maana sana kila mwaka ZIFF inapoanza huwa tunaandamana kuashiria kuanza kwa msimu wa ZIFF."

Majira ya saa kumi na mbili asubuhi kulianzishwa Maandamano ya amani ya kilomita tano yakiongozwa na bendi ya Jeshi la Polisi yakianzia Forodhani, kupitia Darajani, Maisara, Vuga, na kumalizikia Ngome Kongwe Forodhani.

Mwakilishi wa mgeni rasmi, Bi. Asha Ali Hassan akizungumza kwa niaba katika matembezi hayo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI