Na Shemsa Mussa,Kagera.
Naibu katibu Mkuu ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulika na masuala ya elimu Dkt Charles Msonde amezungumza na Maafisa elimu pamoja na Walimu waliokutana katika kumbi za Mikutano Kashozi Sekondari na Bukoba sekondari Mkoani kagera .
Katika vikao hivyo vilivyofanyka nyakati tofauti ndani ya Manispaa na Halmashauri ya Bukoba viliweza kuwakutanisha Maafisa elimu, Wakuu wa shule,Walimu pamoja na wadau wa elimu.
Dkt Msonde amewasisitiza walimu kubadili desturi na mazoea ya ufundishaji na kubuni mbinu mpya za kufundishia ili kuleta ufahulu mzuri na zaidi kwa wanafunzi kimasomo, pia kuwa waadilifu katika nafasi zao za kazi pia kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja.
Amesema ikiwa serikali inaendelea kuzijadili na kuzitatua changamoto za walimu nchini ni vema walimu kuendelea kudumisha tamaduni za kulea na kuwa walezi wazuri kwa wanafunzi.
Pia Dkt Msonde emezitaja changamoto mbalimbali zinazolalamikiwa na walimu kuwa ni kupandishwa daraja pamoja na vyeo kwa walimu baada ya kujiendeleza kielimu (masomo) na kupewa haki zao kulingana na sheria baada ya kuhamishwa pamoja na rikizo.
Dkt Msonde amewaagiza Maafisa elimu wote kuzishughulikia changamoto kwa baadhi ya walimu ambao hawajapata stahiki zao baada ya kumaliza taratibu zote na kutoa mirejesho mizuri kwao.
Nae kaimu Afisa Elimu Mkoa, Mwalimu Honorata Kabunduguru ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Mkoa ametoa shukrani kwa ushirikiano wa walimu na ofisi ya elimu Mkoa na kuwataka walimu kutokukalia kimya changamoto wanazokumbana nazo kazini bila kuzifikisha kwa ( Ma boss) waajili wao.
Nao baadhi wa walimu na wakuu wa shule akiwemo Sadick Revokatuc na Jasnta William wamesema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamuhuli ya Muungano Tanzania Dkt Samia kwa kupunguza na kuondoa baadhi ya changamoto walizokuwa wanakabiliana nazo pia wameiomba serikali kuweka fedha kwa wakati za uendeshaji wa( elimu bure )ili kuepuka changamoto wanazozipata baada ya kuchelewa kupata fedha hizo.
0 Comments