Header Ads Widget

MAKAMISHNA NA MANAIBU KAMISHNA ZIMAMOTO WATAKIWA KUWA WABUNIFU

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini John Masunga amewavisha vyeo Makamishna na Manaibu Kamishna wapatao 12 waliopandishwa vyeo na Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan . 


Pia amewaagiza Makamishna na Naibu Makamishna wa Jeshi hilo la uokoaji waliopandishwa vyeo kuwa wabunifu na kuongeza Kasi ya utendaji kazi ili jeshi hilo liendelee kuwa imara katika utoani huduma.


Masunga ametoa kauli hiyo leo Mei 30,2024 Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma katika hafla ya kuwavisha vyeo na kiapo kwa Makamishna wa Jeshi hilo.



"Nini maana ya kupandishwa cheo, maana yake ni kuongezewa majukumu Rais Dkt Samia aliona nyinyi mnamudu nyongeza ya kuongezewa majukumu kwa hiyo mnapotoka hapa mjue mmeongezewa mzigo wa majukumu"amesema 


Na kuongeza "Tuanpotoka hapa tufahamu kwamba tunaenda kuwatumikia wananchi Kwa kuzingatia viapo vyetu na hiyo ndiyo Dira ya jeshi la zimamoto na uokoaji," Amesema


Akizungumza kwa niaba ya  Makamishna na Manaibu Kamishna wa Jeshi hilo ambao wamepishwa vyeo na kula kiapo Kamishna wa Usalama kwa Umma Athumani Rwahila amesema kuwa wapo tayari kuendelea kufanya kazi usiku na mchana bila kuchoka ili kulinda uaminifu na imani waliopewa ya kuwatumikia wananchi.


Katika hatua nyingine Jeshi hilo limeendelea kuwahimiza wananchi kutoa ushirikiano pindi yanapotokea majanga yenye kuhatarisha Usalama wa maisha ya binadamu na mali zao kwa kupiga Namba 114 ili kupatiwa msaada.




Kwa upande Wake  Kamishina Utawala na Fedha wa Jeshi hilo,Mbaraka Semwanza amemshukuru Rais kwa nishani za Vyeo nakuahidi kufanya kazi kwa utiifu.


"Nina amini hamtomuangusha Rais, nendeni kafanyeni kazi kama mlivyoaminiwa ,"Amewasisitiza


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI