Header Ads Widget

MILIONI 50 KUKARABATI ZAHANATI YA CHOME.



 
NA WILLIUM PAUL, SAME.

HALMASHAURI ya wilaya ya Same katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 imetenga kiasi cha Milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa Zahanati ya Chome ambayo miundombinu yake ni chakavu na kushindwa kukidhi mahitaji ya wananchi kwa sasa.

Akizungumzia changamoto hiyo Diwani wa Kata ya Chome Herieth Makange amesema licha ya uchakavu wa Majengo lakini pia ipo changamoto ya wauguzi ambapo kwa sasa kwenye Zahanati hiyo kuna wafanyakazi wa wili pekee.

Kwa upande wake Momoya George ambaye ni Daktari kwenye Zahanati hiyo anasema pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo lakini hakuna adha ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Zahanati hiyo.

Akiwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero na kutatua malalamiko ya wananchi Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amefika kwenye Zahanati hiyo kujionea hali ilivyo kwa sasa na ambapo pia ametoa maelekezo ya Serikali.

Aidha Kasilda amesema atahakikisha anafuatilia kwa ukaribu fedha hizo zilizotengwa na Halmashauri zinapatkana kwa harakat ili zoezi la kurabati wa miundombinu ya Zahanati hiyo ianze mara moja.

Kata ya Chome ina jumla ya wakazi zaidi ya Elfu tano, huku watu zaidi ya 120 wanakadiliwa kwa mwezi kufika kwenye Zahanati hiyo kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo waja wazito.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI