Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
SPIKA wa Bunge la Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt, Tulia Ackson amefungua maonesho ya Wizara ya ujenzi na Taasisi zake huku akiwakata Mameneja mikoa wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANRODS) kutoa taarifa za haraka kwa barabara ambazo zinahitaji matengenezo ya dharura
Ameyasema hayo Leo Mei 27 ,2024 Bungeni jijini Dodoma huku akisema taarifa hizo za mapema kwa Mameneja hao zitasadia kutotengeneza barabara upya hasa kwenye yale maeneo ambayo wanalazimika kufanya marekebisho
Dkt, Tulia amesema Maonesho hayo yamesaidia wabunge kupata elimu ya uelewa juu ya mtandao wa barabara nchini.
"Na Mimi leo kupitia Maonesho haya nimejifunza hatua mbalimbali hadi kupatikana kwa lami tumeona watu wa maabara namna ya kupima lami vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa kipindi hiki kuanzia mwaka Jana na huu,"
Aidha Dk. Tulia amempongeza Rais Samia kwa kazi nzuri ya uwekezaji wa miundominu "Nimpongeze Rais Dkt Samia suluhu Hassan kwa kazi nzuri anyoifanya hasa kwenye uwekezaji wa miundominu ya barabara kwani kama tunavyofahamu miaka miwili iliyopita Rais Samia alipewa tuzo maalumu ya miundominu kwenye eneo la barabara, " Amesema
Amesema vifaa vya kisasa vilivyonunuliwa hivi karibuni ni vifaa vinayotuondoa kwenye changamoto ambayo ingeweza kupokelewa na wizara.
"Utakuta Mkanadarasi ameshamaliza kazi yake na amekabizi lakini kwa muda ya mwaka mmoja mvua ikinyesha barabara inaleta mashimo hali inayopelekea wabunge kutafakari namna ya kuishauri serikali walipokeaje barabara ya namna hiyo kumbe vifaa vya kupima ubora wa barabara tangia inaanza kujengwa havikuwepo, " Amesema.
Na kuongeza "Nimeona vifaa na magari ambayo inaonyesha wazi barabara hazitopokelewa kabla ya vipimo hivyo basi hatutarajii kuona barabara mpya inamashimo, hatutarajii kuona barabara mpya inatengewa fedha kwa marekebisho," Amesema.
Aidha ametolea mfano barabara ya Iringa Dodoma ni mbovu hali inayopekekea kujengwa upya wakati haina umri wa kujengwa upya.
"Nanaimani vifaa hivi vitakuwa morobaini na Mimi nasisitiza ni muhimu vifaa hivi vikatumike kama vilivyokusidiwa, " Amesema.
Amesema kwa upande wa Tanzania Bara kuna majimbo 214 na hivyo hakuna mahali barabara itapita Mabunge asijue kuwa barabara imekamilika "hatutarajii kuanzia sasa kuona mnapokea barabara kabla hamjapima na zikiharibika mnakuja kuomba fedha kwaajili ya marekebisho. "
0 Comments