Header Ads Widget

WADAU WA KILIMO KANDA YA KASKAZINI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUWAKWAMUA WAKULIMA KUPITIA UMWAGILIAJI.


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Wadau wa kilimo kanda ya Kaskazini wamekutana jijini Arusha katika kongamano la  kujadiliana, kushauriana na kuweka  mipango na mikakati mizuri ya namna ya kuwakwamua wakulima wadogo  katika programu ya umwagiliaji lengo likiwa ni kuwawezesha kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwa na kilimo endelevu.


Akifungua Kongamano hilo lililo andaliwa na kampuni ya Kickstar international mwakilishi wa katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mali mkoa wa Arusha Daniel Loiruk alisema kuwa  wanataka mkulima mdogo na wa kati hasa waliokuwa wakilima tuu bila kujua wanapeleka wapi mazao yao, serikali imeamua kupitia mifumo ya ugani kabla ya kulima waanzie sokoni ndipo waende shambani ili waweze kulima kile kinachohitajika sokoni kwa kiwango na kwa ubora husika ambapo azma hiyo itafanikiwa zaidi kama wakulima wakilima kwa kutumia umwagiliaji.


“Katika hili pembejeo muhimu ni maji  na ni jambo la msingi ambalo kila mmoja wetu katika kila taasisi ambayo imejumuila hapa tukaanza kuunganisha nguvu zetu ili hao wenzetu tunaowaambia wazalishe kwa tija, kwa muda fulani na kwa kulenga soko wawe na njia endelevu ya kufanya kilimo cha umwagiliaji,” Alisema Loiruck.

Alifafanua kuwa tabia ya nchi inagusa maeneo mengi lakini wanachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha kilimo kinakuwa cha mwaka mzima  na sio cha kutegemea mvua peke yake ikiwa ni pamoja na kutoka katika kilimo cha mazoea na kuanza kulima kwa tika kwani maeneo ni madogo na yanazidi kuwa madogo kutokana na ongezeko la watu huku ardhi ikiwa ni ile ile.


“Tunahitaji kuongeza mavuno katika maeneo tuliyonayo na kuongeza tija kwa kuwa na uhakika wa kuvuna bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi lakini pia kuweza kufikia malengo ya agenda ya serikali kuwa ifikapo mwaka 2030 kilimo chetu kiwe kimekuwa kwa zaidi ya asilimia 10.

kwa upande wake Meneja mkazi wa kampuni ya Kickstar international Mwaluko Mpangwa  alisema kuwa dhima kubwa ya shirika lao ni kwainua wakulima wadogo kupitia kilimo cha umwagiliaji ambapo wapo Tanzania kwa takriban miaka 15 na wamewafikia wakulima zaidi ya 64000 sawa na watanzania 300000 kwa kaya.

“Tunaelewa Dunia inapitia changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi, eidha mvua kunyesha chini ya wastani au kunyesha juu ya wastani hali inaleta athari katika mazao ndio maana tumeona  umwagiliaji ni mkombozi kwani tunaamini ni moja ya nyenzo kuu ya kumfanya mkulima kukabiliana na mabadiliko hayo,” Alisema Mpangwa.

Aliendelea kusema kuwa Tanzania ina vyanzo vingi vya maji ikiwemo mito na visima amabapo wanataka mvua zitakapo katika mkulima asisimame bali aendelee na umwagiliaji kwa kutumia teknolojia rahisi na rafiki ambazo wanaweza kuzimudu.


Pia alieleza kuwa bado uelewa wakulima ni mdogo juu ya kilimo cha umwagiliaji kutokana na kilimo cha mazoea jambo ambalo wanapaswa kutoka huko kwani kilimo ni lwa miezi yote 12 kwa kufuata njia bora za kilimo, masoko ambapo wanaendelea kuwapa elimu ili waweze kunufaika na teknolojia na kuleta tija.

Sambamba na hayo Kampuni hiyo ilitambulisha teknolojia ya pampu itayo Money Mekar ambayo ni rahisi kutumiwa na wakulima wadogo kutokana na kuwa rafiki na mazingira, kutokuwa na gharama kubwa lakini kuweza kufanya kazi kubwa ikiwemo kumwagilia hekari 2 kwa siku bila kutumia mafuta wala umeme bali nguvu kidogo na muda wa mkulima.


Aidha baadhi ya wadau wakizungumzia teknolojia hiyo, Mkurugenzi wa shirika la Food for His Children Honorina Honorati linalofanya kazi zake Wilaya ya Karatu alisema kuwa teknojia za umwagiliaji zitarahisisha kazi kwa wanawake kwasababu pamoja na kubadilisha mtazamo kwani kwa kumwagilia kwa ndoo kunapoteza muda mwingi, maji.

“Mwanamke zaidi ya kilimo ana majukumu mengine ambapo teknolojia tulizoona hapa leo zitaokoa muda na kuleta matumizi bora ya maji hivyo nina hamasisha wakulima kutumia teknolojia hizi ambazo hazina gharama kuwa bali manufaa makubwal kwani zina uwezo wa kumwagilia eneo kubwa kwa muda mfupi tofauti na kumwagilia kwa ndoo,” Alisema Bi Honorina.


Afisa ugani kutoka mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji mkoa wa Arusha(Mviwaarusha) Juma Abdilai alisema kuwa  kwa kutumia Pampu zilizotambulishwa na Kickstar international imeweza kuwasaidia wakulima wanaowasimamia kuweza kufanya umwagiliaji na kuweza kuokoa muda, kuwa na matumizi sahihi ya maji pamoja na kuongeza tija kiuchumi na kuwa na chakula cha kutosha na salama.

“Mradi wetu wakilimo ikolojia tunahitaji kuhifadhi kila kitu ikiwemo maji kidogo tuliyonayo na wakulima wetu wameweza kumwagilia mazao yao kwa kutumia teknolojia hii ambayo ni rafiki katika mazingira ya wakulima wadogo ambapo awali walikuwa wakimwagilia kwa ndoo jambo linalotumia muda mwingi lakini pia kuwagilia eneo dogo ambapo kwa sasa wanaweza kumwagilia hekari mbili kwa siku  moja,” Alisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI