MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, ametanagza kutogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika ukurasa wake wa X zamani twitter, Lema, Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kanda za Nyasa, Serengeti na Magharibi.
Kauli hiyo ya Lema, imezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uamuzi wake ambao huku baadhi ya watu wakidai huenda amefanya hivyo kwa hasira baada ya rafiki yake, Mchungaji Peter Msigwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, kubwagwa juzi kwenye uchaguzi wa kanda hiyo.
Msigwa alikuwa akichuana na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), ambaye alimshinda kwa kura 54 dhidi ya 52 alizopata
0 Comments