Header Ads Widget

KUNENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA MKOA HUO KUTENGA FEDHA ZA MICHEZO.

 


 MKOA wa Pwani umezitaka Halmashauri za Mkoa huo kutenga fedha kwa ajili ya michezo ili kuibua na kuendeleza vipaji vya baadaye kwa Taifa.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Rashid Mchatta wakati wa kufungua na kufunga mashindano ya Umoja wa  Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kwenye viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha (KEC).


Kunenge amesema kuwa kutokana na kutokuwa na fedha za kuendeshea mashindano hayo ni vema Halmashauri zikatenga fedha ili ziweze kufanikisha michezo hiyo na ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).


Kwa upande wake kaimu ofisa elimu Mkoa wa Pwani Mashaka Salimu amesema kuwa jumla ya wachezaji 516 na walimu 17 wamechaguliwa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika Mkoani Tabora.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI