Na Ashrack Miraji ,Matukio Daima
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCC Wilaya ya Same CDE. Azza Karisha amewasihi vijana wa kuacha kutumia bodaboda kwa kufanya biashara za haramu ikiwemo kusafirisha dawa za kurevya na kutorosha wanafunzi mashuleni.
Karisha ameyasema hayo wakati akizindua shina la wakereketwa tawi la sokoni Kata ya Same ambapo amesema ni vyema Vijana sasa wajikite zaidi kujitafutia kipato kwa kufanya kazi halali zinazotambulika kisheria.
Kwaupande wake Katibu hamasa UVCCM WIlaya ya Same Salimu Mrutu amesema Vijana wanapaswa kushikamana kwa umoja wao kushirikiana kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Khatibu Joshua Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Same amewaomba Vijana kusimama kwa pamoja kuelekea kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za mitaa kusemea kazi zilizofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa UVCCM WIlaya ya Same amehitimisha ziara yake ya kukagua uhai wa Jumuiya ya Vijana UVCCM na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kuzunguka Kata zote 34 za Wilaya ya Same.
0 Comments