Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
MASHIRIKA ya ndege ya Kimataifa ya Qatar Airways, Emirates na Turkish Airlines kutangaza vivutio vya vivanvyopatikana nchini Tanzania.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki akieleza vipaumbele vya wizara alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jijini Dodoma Leo.
Aidha Mhe. Kairuki alieleza kwamba Wizara itaendelea kutangaza utalii ndani na nje ya Nchi kupitia matangazo katika Ligi na Mashindano ya Michezo yenye wafuatiliaji wengi zaidi Duniani, kutumia watu mashuhuri na wenye ushawishi, Mabalozi wa hiari wa utalii, vyombo vya habari vya Kimataifa vyenye ushawishi pamoja na mitandao ya kimataifa ya utalii kama vile TripAdvisor na Expedia Group, vyombo vya habari kama CNN.
Aidha, Mhe. Kairuki aliongeza kuwa Wizara itaendelea kukamilisha taratibu za kujitangaza kupitia Ligi za Michezo mikubwa Duniani za Marekani na Uingereza na Matukio makubwa ya Burudani.
Vilevile Mhe. Waziri aliongeza kuwa Wizara itaweka mifumo maalum ya mawasiliano katika misitu ya hifadhi ya asili na mashamba ya miti ili kubaini matukio ya moto; na kutoa elimu ya uhifadhi pamoja na kupambana na kuzuia matukio ya moto.
“Katika kuelekea mkutano wa wadau wa Nyuki Kimataifa mwaka 2027 Wizara itaanza utekelezaji wa Programu ya Nyuki kwa Vijana na Wanawake ili kuandaa wataalamu na wajasilisamali wa mazao yatokanayo na asali na mazao mengine ya nyuki” Alisema Mhe. Kairuki.
Aidha, Wizara itaandaa Miongozo na Taratibu za kutwaa na kuhamisha umiliki wa rasilimali za malikale kutoka kwa wamiliki kwenda kwa Wadau kwa ajili ya kuendeleza shughuli za uhifadhi na kuandaa Mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Kale ya Mwaka 2008.
Mhe. Kairuki alisema kuwa wizara itahuisha h muda wa kulipa Ada ya Leseni ya Biashara za utalii na kuwa katika kipindi cha miezi 12 kuanzia siku ya mwisho ambayo wakala wa biashara za utalii amelipia leseni yake badala ya utaratibu wa sasa.
Wizara kwa mwaka ujao wa fedha itapunguza Ada ya Leseni ya Biashara za utalii kwa wakala wa kupandisha wat ofalii mlimani (mountain climbing), kufuta tozo kwa waongoza watalii wenye leseni hai kila wanapoingia hifadhini.
Aidha Mhe. Kairuki alisema kuwa wadau watalipa Ada ya Leseni ya Biashara za utalii kwa kutumia shilingi ya Tanzania badala ya Dola za Marekani pamoja na kuongeza muda wa Leseni ya Biashara za utalii kwa Waongoza watalii ambapo kwa sasa itadumu kwa kipindi cha miaka mitatu badala ya mwaka mmoja wa sasa.
0 Comments