WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. trilioni 10.69 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa yenye urefu wa kilometa 1,219 kuanzia Dar es Saalam hadi Mwanza.
Akielezea utekelezaji wa miradi nane ya kielelezo kwa mwaka 2023/2024 Bungeni Jumatano, Aprili 3, 2024, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Februari 2024, ujenzi wa reli hiyo umefikia viwango vya kati ya asilimia 5.38 na asilimia 98.84, tayari reli hiyo imeshaanza kufanyiwa majaribio kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.
0 Comments