Header Ads Widget

WAHITIMU UDSM FIVE CLASS 2007 WANA JAMBO LAO

   WAHITIMU WA UDSM FIVE 2007 ENZI HIZO WAKIWA MASOMONI

Na Mwandishi wetu, Matukio Daima App, Dar es salaam

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) five Class 2007 wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam kubadilishana mawazo na kushirikishana fursa mbalimbali za maendeleo.


Akizungumza na MATUKIODAIMA App leo April 30,2024 jijini Dar es Salaam, kiongozi wa wahitimu hao, Frank Gwaluma amesema kikao hicho kitafanyika The Deck Kitchen & Bar iliyopo Masaki karibu na Kambi ya Jeshi Mei 24,mwaka huu.


    FRANK GWALUMA KIONGOZI WA WAHITIMU HAO


Amesema lengo kubwa la kikao hicho ni kukumbushana walikotoka na kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kushirikishana fursa za maendeleo.

"Ni kikao cha kawaida tumekiandaa sisi tuliokuwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Facult ya Informatics and Virtual Education (FIVE) kwa sasa College of ICT (CoICT).

"Tukizingatia ni muda mrefu umepita hatujakutana. Hivyo tumeona huu ni wakati muafaka kwetu kujumuika, kufurahi pamoja na kujadiliana fursa za maendeleo, hili ndilo lengo letu hasa.

"Nichukue fursa hii kuwakaribisha wenzetu wote ambao tulisoma pamoja lakini kwa sababu mbalimbali hatuna mawasiliano nao wajue tupo na tunawahitaji sana wajumuike nasi" amesema Gwaluma.

Kuhusu mgeni rasmi, Gwaluma amesema wanatarajia kuwa na baadhi ya walimu waliowafundisha chuoni hapo na humo ndipo atapatikana mgeni maalum.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI