Header Ads Widget

MTUHUMIWA MMOJA KATI YA WATATU WA MAUAJI YA MWENYEKITI WA KITONGOJI ANASWA NA POLISI.



NA WILLIUM PAUL, SAME. 



Pamoja na mtuhumiwa mmoja kati ya watatu wa tukio la mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sinangoa "A" Kata ya Ndungu Tarafa ya Ndungu Jimbo la Same Mashariki kukamatwa, Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Kasilda Mgeni ameagiza Jeshi la Polisi kufanya oparesheni maalum ya kuwasaka na kuwakamata haraka watu wote walioshiriki kupanga njama na kuteleza maujai hayo ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.



Tukio la maujai ya Mwenyekiti huyo Ndugu. Charles Mkuruto  (58) limetokea April 26 mwaka huu akiwa kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi baada ya kuvamiwa na kushambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani na nyuma ya bega la kulia na watu watatu wa familia Moja.



DC Mhe. Kasilda ametoa agizo hilo wakati akitoa neno la Serikali kwa waombolezaji, ambapo amewaonya wananchi kutolipiza kisasi na kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake waiachie Serikali iendelee kutekeleza wajibu wake kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa na kufikishwa kwenye mamlaka husika waweze kupatiwa haki yao.



"Mimi Mkuu wa Wilaya ya Same na Kamati yangu ya Usalama tumesikitishwa sana na mauaji haya ya kikatili ya Kiongozi wetu wa Serikali mwadilifu Ndugu Charles Mkuruto ambaye Serikali na wananchi wamemuamini na kumchagua kuongoza kwenye kitongoji hiki cha Sinangoa "A", niseme tu wananchi wangu matukio haya hayakubariki na siyo sawa kabisa kutendeana".



Marehemu Charles ameacha mke mmoja na watoto wawili wa kike pamoja na wajukuu wa wili, mbali na kuwa mtendaji Serikalini, Ndug. Mkuruto alikuwa pia Kiongozi wa kaya na familia, mkuu wa huduma, shemasi mkuu, Kiongozi wa uwakili pamoja na amo katika kanisa la Adventist wasabato Ndungu Central Jimbo la Same Mashariki hadi umauti ulipo mkuta April 26 2024.



*"Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe"*.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS