Header Ads Widget

UMOJA WA MADHEHEBU YA KIKRISTO WALIOMBEA TAIFA










Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

 

UMOJA wa Madhehebu ya Kikristo umefamya ibada ya kuliombea Taifa la Tanzania huku Mgeni Rasmi akiwa mkuu wa Mkoa huo aliyewakirishwa na Mkuu wa Wilya wa Chamwino Janeth Mayanja.


Ibada hiyo ilifanyika Aprili 1,2024 jijini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri ambapo akiwasilisha Salamu za Mkuu wa Mkoa Mayanja ameipongeza kamati hiyo ya maandalizi kwa kutoa ushirikiano wa hali na Mali kwa serikali hali inayosababisha shughuli za Mkoa kwenyika kwa urahisi.


Ameupongeza umoja huo kwa kuwa na Ubunifu wa Kuombea Nchi na Familia kwa lengo la kuhakikisha haki, Amani na Upendo vinadumu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.


Mayanja amewakumbusha Viongozi wa Dini kuhakikisha wanaendeleza vipindi vya Watoto makanisani kwa Lengo la kuendelea kufundisha vijana na Watoto umimu wa kulinda na kuyadumisha Maadili mema.


“wakati ninyi mnaikumbusha serikali kuhusu kusimamia maadili ili kuwakinga watoto wetu na Mmomonyoko wa Maadili unaotokana na utandawazi uliyopo katika jamii ya watanzania, na mimi niwaombe kuendeleza vipindi vya vijana na Watoto katika makanisa vitavyowajenga Watoto katika maadili mema,


Tuwekeze nguvu kubwa katika kuwajenga Watoto na vijana wetu, katika maadili bora badala ya kuhangaika na watu wazima kwani Samaki mkunje angali mbichi, tukawambie kuhusu ubaya wa vitendo vya Ushoga, usagaji, ubakaji, matumizi ya vilevi, madawa ya kulevya, chuki, visasi na migogoro isiyona tija, badala yake wakawe watu wema katika jamii na kwa njia hiyo tutakuwa tumelijenga taifa Bora la Watanzania”, amesema


Pamoja na kuwapa Watoto elimu ya Dunia lakini pia tuhakikishe tunawafundisha elimu ya Dini, hasa siku za mwisho wa wiki ambazo Watoto wanakuwa mapuziko wasiishie kuangalia katuni kwenye Tv au magemu kwenye simu badala yake jamii iwafunze Watoto elimu ya Dini.


Katika hatua Nyingine DC huyo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu hassani kwa kuwatengenezea watendaji wa serikali mazingira mazuri katika maeneo yao ya kazi kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya kimaendeleo, tofauti na vipindi vya Nyuma ambavyo walikuwa wanapata kigugumizi hata kufanya ziara vijijini kwa kuhofia kuulizwa maswali yasiyo na majibu.


“rais Samia ametufanya watetendaji wa serikali na wateule wake tuwe na ujasiri wa kufanya ziara kila mahali bila kuhofia kuulizwa maswali na wananchi yasiyo na majibu, kwani kila unapokanyaga unakuta Mradi uwe wa Elimu, maji, afya, Umeme au miundombinu ya Barabara unatekelezwa hakika ameweka historia kubwa katika uongozi wake kwa kutatua kero za wananchi”, amesema Mayanja


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madhehebu ya Kikristo yayounganisha TEC, CPCT na CCT, Anthon Mjashimba ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Babtist kanda ya kati, amesema katika Mkoa wa Dodoma hakuna Shari wala Swali katika umoja huo.


“umoja wa madhehebu ya kikristo mkoani kwetu hakuna ile nani bora au nani siyo bora katika ibada zetu, sisi sote ni kitu kimoja tumepatana kufanya kwa Pamoja, ndiyo maana tunakutana kufanya maombezi kwa ajili ya taifa, serikali, viongozi na jamii kwa ujumla pia tunafanya makongamano mbalimbali na hata mwezi wa saba mwaka huu tunakutanisha kwaya zetu Zaidi ya 100 kwenye tamasha moja”. Amesema


Amesema lengo la Ibada ya Pasaka pili ni Kukumbuka kifo na kufufuka kwa Yesu Mkombozi wa Ulimwengu, Lengo la Pili likiwa ni kuliombea Taifa ili haki ikatendeke kwenye Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa Mwaka Ujao ili taifa livuke salama.


Nae Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCT, Tanzania ambeye ni mratibu wa Shughuli za Wanawake na Watoto, Magreth  Masawa amewashauri wanawake ambao wana jukumu kubwa la malezi ya familia kuhakikisha wanawafundisha kwa kuwasemesha Watoto wao tangu siku ya kwanza ya kutunga mimba Pamoja na kuwaombea waweze kuwa katika maadili mema yenye kumpendeza Mung una jamii kwa ujumala.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI