Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 02.04.2024

 


Newcastle wanatarajiwa kurejelea azma yao ya kumnunua mlinda lango wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 25, msimu huu wa joto huku wakimlenga kipa mwenye umri mdogo zaidi. (Mail)

Newcastle wanajiandaa kupokea ofa kutoka kwa Arsenal na Tottenham, ambazo huenda zikagharimu pauni milioni 100, kwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, huku vilabu vikitazamia kuchukua fursa ya hitaji la Magpies kutafuta fedha za kuwaruhusu kurejesha kikosi chao ndani ya sheria za usawa wa kifedha. (Sun)

Tottenham na Newcastle wameambiwa watalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 50 iwapo wanataka kumsajili kiungo wa zamani wa England wa chini ya miaka 21 Morgan Gibbs-White, 24, kutoka Nottingham Forest, ambaye huenda akalazimika kumuuza kwa sababu ya matatizo yao ya kifedha. (Football Insider)

    Mshambuliaji wa Uswidi na Newcastle Alexander Isak


West Ham italazimika kulipa pauni milioni 60 kama wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 22. (Football Insider)

Manchester City wanatarajiwa kumweka kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kwa uhamisho wa kudumu msimu wa joto kwa bei ya pauni milioni 30. (Mail)

Liverpool, Tottenham na AC Milan wako tayari kupigania saini ya beki wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Sun)

Real Madrid wanatathmini uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa Chelsea na England Reece James lakini wanatarajia dili lolote kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa gumu kwa sababu amesalia na miaka minne kumaliza mkataba wake. (Fichajes - kwa Kihispania)


Beki wa Barcelona na Uhispania Marcos Alonso, 33, anatarajiwa kuondoka bila malipo msimu huu wa joto, huku kiungo wa kati wa Uhispania na beki wa pembeni Sergi Roberto pia akaondoka bila malipo. (Fabrizio Romano)

Nyota wa zamani wa Barcelona na Paris St-Germain Neymar, 32, anapanga kurejea kwao Brazil na Santos mnamo 2025 mkataba wake na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia utakapomalizika. (Goal)

Barcelona wamesitisha mpango wa kumnunua Estevao Willian, 17 wa Palmeiras na Brazil ambaye amepewa jina la 'Messinho', katika hatua inayotoa nafasi kwa Chelsea na Paris St-Germain kumsajili. (Sport - kwa Kihispania)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI