Header Ads Widget

PROF. MKENDA "MGAWANYO WA FEDHA ZINAZITOLEWA NA SERIKALI ROMBO HAUFANYIKI KWA UPENDELEO"



NA WILLIUM PAUL, ROMBO.


MBUNGE wa Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia,  Profesa Adolf Mkenda amesema mgawanyo wa fedha zinazotolewa na serikali katika tarafa mbalimbali ndani ya wilaya ya Rombo haufanywi kwa upendeleo bali kwa kuzingatia uhitaji katika kila eneo.


Pia amesema kwa kipindi Cha miaka 3 , serikali imetenga mamilioni  ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilayani hiyo ikilinganishwa na kipindi cha Miaka 10 iliyopita.



Profesa Mkenda alisema hayo wakati akifanya mkutano wa ndani na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya CCM kutoka katika Tarafa ya Mengwe kuelezea maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita wilayani Rombo kwa kipindi cha miaka mitatu  chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumzia mgawanyo huo wa fedha zilizotolewa na serikali  kupitia halmashauri  kwa kipindi cha miaka 3 Profesa Mkenda amesema ,  Tarafa ya Mkuu ilipata kiasi Cha bilioni 3.8, Mengwe bilioni 3.558, Tarakea bilioni 2.3 , Useri bilioni 2.419 huku Mashati ikipata zaidi ya kiasi Cha shilingi milioni 903.



Pia mewataka Viongozi hao wa ngazi mbalimbali wakiwemo  Wenyeviti wa Kitongoji , vijiji na kata pamoja na makatibu wa CCM kata na makatibu  wenezi wa chama kata kuepukana na propaganda ambazo zinakiharibu chama na kuchelewesha maendeleo.


Awali akizungumza Katibu wa CCM wilaya ya Rombo, Mary Sulle amewataka Viongozi hao kuepuka na kuachana na tabia za kiuchonganishi kwa Viongozi wao kwani  zinasababisha kudhoofisha maendeleo.



Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mwangala pamoja na kumpongeza Mbunge Profesa Mkenda kwa maendeleo anayosababisha Rombo , amewataka Wananchi wa Rombo kushirikiana pia kuhakikisha wanapanda miti kwa bidiii Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .



Akizungumza athari za mafuriko kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha amesema pamoja na  wananchi Wilaya ya Rombo kutokukubwa na  madhara,  amewataka kuhakikisha wanaotoa taarifa pale wanapoona dalili za mafuriko kwani ni bora kuzuia majanga Ili kuepukana na madhara.

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS