Header Ads Widget

FCC YAISHUKURU SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI

 

Na Fatma Ally Matukio na Habari App

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Nchini (FCC) Hadija Juma Ngasongwa amesema tume hiyo, inajivunia na kuishukuru  Serikali kuweza kutengeneza mazingira rafiki  ya wawekezaji kuhakikisha mwekezaji wa ndani anaweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali.

Hayo ameyasema wakati alipotembelea banda la Viwanda na Biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara kimataifa (Sabasaba) ambapo amesema FCC itaendelea kutimiza maagizo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuimarisha hali ya biashara nchini.

Aidha amesema, wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji ili kusaidia kulinda na kuimarisha biashara zao.

"Lengo la kuanzishwa kwa Tume ya Ushindani(FCC) ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara kati ya kampuni na kampuni,pamoja na kudhibiti bidhaa bandia."amesema Ngasongwa


Hata hivyo, amesema lengo kubwa ni kuhakikisha wawekezaji ndani ya nchi waone kwamba kuna sheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanao ufanya."


Sambamba na hayo ameongezea kuwa kushiriki kwao katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kubwa,huku akiwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho hayo kuchangamkia fursa za uwekezaji kwani  kuna zaidi ya makampuni 3000 yanayo patikana kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara viwanda.


Ameeleza kuwa kuna sheria ambayo ina thibiti bidhaa bandia,nakwamba ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la Wizara hiyoili waweze kujua namna ya  kutofautisha bidhaa bandia na bidhaa halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu elimu hiyo.


Amesema kuwa mwekezaji Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwekezaji  mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara kwa pamoja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI