Header Ads Widget

MADAKTARI BINGWA WA MOYO KUPIGA KAMBI KIGOMA

 




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MADAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyo chini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wanatarajia kuendesha kliniki ya siku tatu ya upimaji na kutibu hatua za awali za magonjwa ya moyo kwa  wananchi wa mkoa Kigoma.

 

Afisa Habari na mahusiano kwa umma wa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni, Syprian Sophanius alisema kuwa kliniki hiyo itaanza April 16 hadi 18 mwaka huu kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la watu wa Marekani (USAID).

 

Sophinius alisema kuwa madaktari bingwa wanne wa moyo kutoka JKCI watashiriki kliniki

hiyo wakisaidiwa na wataalam wa tiba kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni watatoa huduma kwenye kliniki hiyo.

 

Katika taarifa yake Afisa Habari huyo alisema kuwa watakaobainika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi Zaidi na kufanyiwa matibababu hapo hapo Hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni na wale watakaobainika kuwa na matatizo makubwa Zaidi watapewa rufaa Kwenda JKCI kwa matibabu Zaidi.

 

Kliniki hiyo inayojulikana kama Mama Samia Outreach Services itatolewa bure kwa wananchi watakaofika kuonana na madaktari hao kutochajiwa gharama zozote.

 

Kwa mujibu wa afisa Habari wa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma alisema kuwa kambi hiyo ya matibabu ni sehemu ya uzinduzi wa mradi wa lishe utakazinduliwa April 18 ambao unaendeshwa kwa ufadhili wa USAID.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI