Header Ads Widget

ARUSHA YA CHANGIA ASILIMIA 57 YA MAPATO YA UTALII NCHINI KWA 2022/2023

Na, Matukio Daima App,



Imeelezwa kuwa asilimia 57 ya mapato yote ya Utalii yaliyopatikana katika mbuga za wanyama mwaka 2022/23 yalitokana na vivutio vinavyopatikana Arusha na Kanda ya Kaskazini kwa Ujumla na hii ni kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Ripoti hiyo ya Uchumi wa Kikanda imeonyesha kuwa kuongoza kwa kanda ya kaskazini iliyo na Kitovu chake jijini Arusha kunatokana na idadi kubwa ya watalii kuchagua eneo la Kaskazini kama sehemu yao kuu ya Kupumzikia.

Uchambuzi umeonyesha pia, zaidi ya Tsh. Bilioni 463.34 zilipatikana kupitia watu mbalimbali waliotembelea mbuga hizo ikiwa ni ongezeko la asilimia 43.4 ikilinganishwa na Tsh. Bilioni 323.2 zilizopatikana katika kipindi kama hicho Mwaka uliotangulia.

Hata hivyo, taarifa hii inakuja wakati mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda akitangaza lengo lake la kusimamia agizo la Mh. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan ambalo ni pamoja na kukuza na kutunza sifa hiyo nzuri kwa Mkoa wa Arusha ili kuendelea kuwa Kinara Katika kuliingizia Taifa fedha nyingi za Kigeni.
 

Katika kutekeleza suala hilo tayari ameanza kukutana na wadau mbalimbali wa Utalii ili kuwasikiliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kuzitatua ili kuhakikisha wanafanya kazi zao bila ya Vikwazo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS