Header Ads Widget

TYCS NJOMBE WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati wanafunzi wa kidato cha sita wakitarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mwezi Mei mwaka huu,Wahitimu wametakiwa kuzingatia maadili,Nidhamu na weledi mkubwa pamoja na kumtanguliza mungu.


Katika mahafali ya Kidini ya Wanafunzi wa Dhehebu la Roman Katholi TYCS kidato cha sita kwa shule za sekondari Njombe(NJOSS) Uwemba na Wanike yaliyofanyika Njoss Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amewataka wahitimu hao kutambua kuwa utovu wa nidhamu unasababishwa na kutokuwa na Imani thabiti.


Aidha Mpete ameonya dhidi ya mmomonyoko wa maadili unaochagiza kuwapo kwa  mapenzi ya jinsi moja huku akiwataka walimu kuwaacha wanafunzi wasome badala ya kuwarubuni.


Flatel Mtega ni mseminari toka Parokia ya Njombe ambaye anasisitiza wanafunzi kuzingatia masomo ili wazifikie ndoto zao.


Katika taarifa ya wahitimu hao iliyosomwa na Joachim Shayo imeeleza kuwa nidhamu ndio nguzo ya mafanikio yao na kwamba wamekuwa wakifanya vyema katika mitihani kutokana na Kuzingatia maadili mema.


Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa shule ya sekondari Njombe makamu wa shule hiyo Mwalimu Melkisedeck Mbata amewataka wanafunzi kwenda kufanyia kazi nasaha zilizotolewa.


Mshike sana elimu wala usimuache aende zake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI