Header Ads Widget

NFRA WATAKIWA KUONGEZA NGUVU YA UNUNUZI WA MAHINDI NJOMBE






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakala wa hifadhi ya Chakula nchini NFRA Umetakiwa kuongeza nguvu katika ununuzi wa mahindi ya wakulima mkoani Njombe kwani wakulima wanapata hasara kubwa kwa kulanguliwa mazao yao.


Katika kikao cha wadau wa kilimo kilichoandaliwa na Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) chini ya mradi uliolenga kusaidia taasisi za wakulima kwa nchi za Afrika, Caribean na Pacific ,Four Four ACP(F04ACP) kilichofanyika  mkoani Njombe Baadhi ya wakulima hao toka   vyama vya msingi akiwemo Yohane Mhagama na Stephano Luoga wameomba  NFRA Waongeze nguvu katika ununuzi wa mahindi yao kwani wanapata hasara kubwa ukilinganisha na gharama za uendeshaji.


Weledi kwa viongozi wa vyama vya ushirika ni wito unaotolewa na Kaimu mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Njombe bwana Fredy David ambaye ni Ofisa ushirika halmashauri ya wilaya ya Njombe.


Katibu mtendaji wa Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) Florian Haule amevitaka vyama vya ushirika  kujiendesha kibiashara na kuacha kufanya shughuli zao kwa mazoea bali mikutano na vikao vitumike kuibua fursa mpya.


Mratibu wa mradi wa FO4ACP Bwana Peter Mtenda  toka shirikisho la vyama vya ushirika nchini amesema wanauona mwanga baada ya mkutano huo katika pande zote kwani wanaamini wakulima wataenda kupata suluhu la soko katika mazao yao.


Afisa Ubora Wakala wa Taifa hifadhi ya chakula (NFRA) Makambako Josephat Ringo amekiri kupokea maombi ya wakulima hao huku akiwasisitiza kuzingatia ubora katika mazao yao.


Ringo amesema wao huwa wanatoa mikataba na kipaumbele huwa ni kwa vyama vya ushirika lakini changamoto inayojitokeza ni kuwa uzalishaji unatofautiana kulingana na majira.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI