Header Ads Widget

MAAJABU YA BEI VYAKULA VYA MFUNGO WA RAMADHAN NA KWARESMA IRINGA ,BEI YA DAGAA MARA MBILI ZAIDI BEI YA NYAMA



WAKATI  waumini  wa  dini  ya  kiislamu  wakiwa  katika mfungo  wa  mwezi  mtukufu  wa  Ramadhan  na  wakristo  wakiwa  katika  mfungo  wa  Kwaresma  bei ya    vyakula  katika  soko  kuu la Manispaa  ya  Iringa  imeendelea  kuwa  rafiki  kwa  wafungaji  hao  huku  bei ya  dagaa nyama nono ikipanda  zaidi kwa  kilo kuuzwa  kwa  Tsh  20,000 ukilinganisha na  kilo ya  nyama  inayouzwa  Tsh 8000.

Akizungumza na Matukio Daima Media  Mariam  Mahige  ambae  ni mfanyabiashara  wa  Dagaa katika  soko  kuu la mkoa  wa  Iringa  soko la  Manispaa ya  Iringa   alisema  kuwa  bei  ya  dagaa hizo maarufu  kwa jina la Nyama Nono  kutoka Mwanza  imekuwa juu  kutokana na upatikanaji  wake  kuwa  mgumu na  kuwa awali  dagaa hizo zilikuwa  zikiuzwa  kati ya Tsh 14,000 hadi 17,000 ila  kwa  sasa  zimekuwa adimu  zaidi  kutokana na walaji  wengi  kupenda  kuzitumia .

Hata  hivyo  alisema  dagaa nyingine kama aina ya  Fulu na  nyingine  zinauzwa     Tsh 16,000  pia  dagaa hizo  zinawawalaji  wengi  kwani  wateja  wa  jumla wanakimbilia  kununua  dagaa  hizo  aina ya  Fulu  ambazo pia  zinatoka  Mwanza .


Ngowi  Msungu ni mfanyabiashara wa  Samaki  katika  soko  hilo  alisema  bei ya  Samaki  wa kati  ni Tsh  500 kwa  mdogo  kabisa na Samaki wa kati ni Tsh 5000 na  kuwa  Samaki  wakubwa zaidi  hawapatikani  kirahisi  na kuwa  Samaki  wa Tsh 5000 ni  yule ambae  wakati wa  samaki  wengi alikuwa akiuzwa kati ya shilingi 2500 hadi 3000 ila  idadi kubwa ya  walaji wa samaki  wamekuwa  wakilazimika  kununua Samaki  wachanga   wanaopangwa  kwenye mafungu  kwa  kuuzwa  shilingi 1000 hadi 2000.

Wakati  bei ya  nyama  katika  maduka  ya nyama  (Bucha)mjini  hapa  kilo  moja  ikiuzwa  Tsh 8000 na  kilo  moja ya  utumbo  ikiuzwa 6000 Maharage  kwa  kilo  yamekuwa  yakiuzwa  kati ya  shilingi  3000 hadi 2000  tofauti na  miezi  mitatu  nyuma  wakati  bei ya  maharage   ilikuwa ikiuzwa hadi  shilingi 2100 hadi 2200  alisema  mfanyabiashara  John  Sanga  kuwa  bei ya maharage  haijapanda  kama  wakati  wa miezi ya  Kilimo ambayo  walaji  walikuwa ni  wengi  kutokana na uhitaji  wa mbegu na  sasa  sehemu  kubwa maharage wakulima  wameanza  kuvuna .

Sanjari na  bei ya  mboga hizo  ambazo  hutumika katika  mfungo  wa kwaresma na mwezi  mtukufu wa Ramadhani  pia bei ya   mchele kwa  kilo katika  soko  hilo imekuwa  ikiuzwa kati  ya shilingi 2100 hadi 2800  tofauti na  siku  za  nyuma ambapo  mchele  ulikuwa kati ya  shilingi 1700 hadi 2000.

 

Wakati  unga kwa  kilo 25 ukiuzwa  Tsh 30000 na  kilo  5  ukiuzwa  Tsh 7000  bei  ambazo  zilikuwa  zikitumika wakati  wote  alisema  Maria John  mfanyabiashara  wa mchele na  unga  sokoni  hapo .


Mfanyabiashara  wa  ndizi  na viazi mviringo  katika  soko  hilo Hamida Kihongosi  alisema  bei ya  ndizi  mkungu ni kati ya  shilingi 17000 na  ndizi  mzuzu  zikiuzwa  Tsh  30,000 bei  ambayo  wamekuwa  wakiuza wakati  wote   wakati  viazi  kwa  debe  la  lita  20 vikiuzwa  tsh 15,000 na  gunia  wao  wakinunua  Tsh  60,000.

 

Wafanyabiashara  wa Mihogo ,magimbi na viazi  utamu  sokoni  hapo Isaya  Mbalingwa na Obadia Isaya  pamoja na Abnel  Chuma  walisema  kuwa  bei ya vyakula  hivyo  imekuwa ikiyumbishwa na hali ya upatikanaji  wake  kwa mfano  mihogo ya  Pawaga  Iringa bei yake  imekuwa  kubwa ukilinganisha na  mihogo ya  Morogoro  ambayo ina  asili ya Kamba  hivyo bei  yake ni  ndogo  zaidi na kuwa bei ya  mhogo  mmoja  ni kati ya  shilingi 1500 na  2000 bei  ambayo  haina tofauti na  kabla ya  kuanza kwa mfungu   wakati boga  moja  likiuzwa  Tsh 2000 hadi  3000 .


Hata  hivyo  bei ya  tambi  kwa  kilo  moja katika  soko  hilo  ikiwa  juu  zaidi  kwa  kuuzwa  Tsh 30000 ukilinganisha  na miezi  miwili  nyuma  ambapo  tambi  ziliuzwa tsh 20,000 hadi 27,000 kwa  kwa  kilo .

Pamoja na  wafanyabiashara  wa vyakula   hizo  zinavyohusika  na  mfungo  kudai  kuwa  bei ni kawaida  baadhi ya  wateja  walisema  bei  hiyo ni kubwa ukilinganisha na hali  halisi ya Maisha  ya  sasa  kwani mhogo  ambao  umekuwa  msaada mkubwa kwa wale waliopo  kwenye mfungo  bei yake  si  rafiki kwa mlaji tofauti na  mwaka  jana  wakati kama  huu wa mfungo mhogo  ulikuwa kati ya shilingi 500 hadi 1500 bei  ambayo haikuwa  mbaya  zaidi  alisema Eliasa Juma .

Kuwa ni  vema  bidhaa  hizo  za  mfungo  kutazamwa  kwa  jicho la tatu  ili  zisimjuumize  mlaji kwani hali ya  upatikanaji  pesa  mfukoni  si nzuri  sana .

Monica Kalinga  alisema  bei ya  vyakula  si mbaya  sana  ila bei ya  mboga  mboga  mfano  dagaa ,Samaki ipo  juu  sana kwani kwa  kawaida  dagaa ni  mboga  ya hali ya  chini  ambayo  awali  ilikuwa  kimbilio kwa  wenye  kipato  cha  nchini  ila  leo  dagaa  zimekuwa bei  juu  zaidi  kuliko hata  nyama jambo  ambalo  linashangaza  zaidi  kuona kilo moja ya  dagaa  ikiuzwa  Tsh 20000 wakati  nyama  ikiuzwa  Tsh 8000.

 


Akielezea  hali  halisi ya  bei ya  bidhaa sokoni  hapo mwenyekiti wa Soko kuu la  Iringa Raphael Ngulo  alisema wanaishukuru  serikali kwa  kuthibiti upandaji  holela  wa  bei katika masoko kwani  bei ya  vyakula vya  mfungo ndani ya  soko  hilo haijapanda  sana  ukilinganisha na miaka mingine .

Alisema  ukiona bidhaa imepanda  bei  zaidi  ni kutokana na upatikanaji  wake  kuwa mgumu  kwa  baadhi ya maeneo miundo  mbinu ya  Barabara  kuharibiwa na mvua  hivyo  kupelekea  bidhaa kushindwa  kutolewa  mashambani  na zile  zinazofanikiwa  kutolewa huuzwa kwa  bei  ya juu  zaidi .

Hata   hivyo  alisema bei ya  bidhaa za wafungaji  wote  zimekuwa  rafiki  zaidi mfano sukari  ambayo ni hitaji  kubwa kwa  wafungaji  hivi sasa  inauzwa  kati ya  shilingi 3200 hadi 2800 tofauti na awali  ilipokuwa  ikiuzwa Tsh 6000 hadi 7000.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI