Header Ads Widget

UNDP YAZINDUA WAZO LA KIBUNIFU LA MATUMIZI BORA YA NISHATI NCHINI.

 



Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima app Dodoma

SERIKALI  kupitia Wizara ya Nishati imeshuhudia uzinduzi wa  Mpango wa matumizi ya nishati Bora Tanzania unaoenda Sanjari na Mradi  wa wazo la kibunifu la matumizi sahihi ya Nishati ambalo litagharimu jumla  ya  Shilingi Milioni250 kwa washiriki ambao watachaguliwa  kushiriki kuandaa kazi zao ambazo zitaleta suluhisho la changamoto ya matumuzi yasiyo sahihi ya nishati


Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma katika uzinduzihuo,kwaniaba ya Kamishina  Maaidizi wa  Nishati ya Umeme,Mhandisi Collins Rwanga amesema Serikaliinaunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la kimataifa la UNDP.


"Niwaombe watanzania wote kuchangamkia fursa hii ya wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati , " Amesema 


Na kuongeza"Tumekuja kushuhudia uzinduzi wa shindano la wazo la kibunifu kuhusu matumizi bora ya nishati nchini ningependa kuwaalika watanzania wote kuweza kushiriki na kuendelea kubuni bunifu zenye tija kwani kila mmoja anatambua umuhimu wa sekta hii ya nishati"Ameongeza Lwanga


Kwa upande Wake Mhandisi Robert Washaija ambaye ni Mtaalam mashauri wa Shirika la maendeleo la Kimataifa la UNDP amesema shirika hilo,kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Umoja wa Ulaya na Nchi ya Irelish Ni Mpango Mkakati wa matumizi Bora ya Nishati lengo lilies ni kuhakikisha Nchi  iliyopo kwenye Uchumi wakati wa Viwanda inakuwa na matumizi Bora ya Nishati.


Washaija amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kwamba Tanzania kama nchi inakuwa na matumizi bora ya Nishati kwa sababu nishati ni kitu bora katika maendeleo ya viwanda


"Mradi huu kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na wafadhili wetu umoja wa Ulaya tunafanya Kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Viwanda, Tunafanya Kazi na Shirika la Viwango Tanzania TBS, Tunafanya Kazi na Takwimu NBS, Tunafanya Kazi na taasisi ya elimu DIT na ni mradi ambao ni mpana sana na unalenga maeneo makubwa Sana"Amesema Washaija


Aidha amesema kuwa moja ya matunda ya mradi huo ni Kujenga uwezo nchini na kuwa na wataalamu wa kisasa ambao wataweza kutoa huduma mbalimbali pale zinapohitajika kuhusu matumizi bora ya Nishati,na kuzijengea uwezo Taasisi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake.


" Tunatambua kwamba eneo hili ni geni kwani tukianzia majumbani ni wengi wanapoteza nishati kwa kushindwa kutumia nishati  kwa usanifu na kuweza kutumia nishati kubwa na kuipoteza kwani tungekuwa tunafuata matumizi bora ya nishati tusingekuwa na mgao wa umeme kama tungekuwa na matumizi rasmi ya umeme"Amesisitiza Washaija


Akielezea kuhusiana na Shindani hilo la kibunifu,Jolson Masaki Mchambuzi  wa Mawasiliano,amesema Shindano  litahusisha Watanzania wote wakiwemo Vijana amesema  watachukua  bunifu 10 ambazo zitalenga kupunguza matumizi ya nishati zisizo sahihi lengo likiwa ni kuongeza uelewa kwa Jamii.


Amesema kuwa kwenye shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini wanalenga zaidi vijana wakike na wakiume wenye mawazo ya kibunifu yanayoenda kutoa mchango mkubwa katika kupunguza matumizi ya Nishati


"Ninaposema kupunguza matumizi ya Nishati ina maana kwamba kuna Nishati ambayo tunaitumia vibaya,sasa kupitia mawazo hayo ya kibunifu tutaenda kupokea maoni kutoka kwa Watanzania"Amesema Masaki


Aidha amesema kuwa ili uweze kushiriki katika shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati kitu cha Kwanza lazima uwe na wazo la kibunifu ambalo linahusiana na matumizi bora ya Nishati,Lazima uwe Mtanzania na washindi kumi watachaguliwa ambapo katika hao washindi watapata Milioni Ishirini na tano kwa kila mmoja.


Ameongeza kuwa katika mawazo hayo ya kibunifu wanatazamia kupokea mawazo ambayo yanaweza kupunguza matumizi ya Nishati na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa yakiathiri nchi zetu.


Pia Masaki amesema kuwa wazo hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati ambalo litakuwa ni la mda wa mwezi mmoja .


Kuhusu mwendelezo wa hili shindano la kibunifu la matumizi bora ya Nishati Masaki amesema kuwa huu mradi ni wa muda wa miaka mitatu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI