Na Mwandishi wetu Kilwa Matukio app Mtwara
Uwekezaji uliofanyika kwa serikali kutoa Sh 1.4 Bilioni ya kuchochea ongezeko la Watalii kutembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara vilivyopo Wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilitembelea maeneo hayo Machi 14 .2024 ya Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwa lengo la kwenda kukagua Utegelezaji wa Miradi ya Utalii katika hifadhi hiyo.
Miradi takribani 9 imetekelenzwa katika maeneo hayo ikiwepo kununuliwa kwa Boti ya kisasa yakutembeza watalii,njia yakupita watalii,Jengo la kupokelea na maeneo mengine.
Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amesema idadi ya Watalii wanaofika Kilwa Kisiwani imeongezeka tofauti na miaka ya 2018-9 ambapo watalii takribani 2988 ndiyo waliokuwa wakitembelea Hifadhi hiyo.
"Idadi ya watalii imeongezeka mwaka 2018-19 walikuwa wanafika watalii takribani 2988 lakini kwa sasa idadi inafika hadi zaidi ya 6000,Kwa mwaka huu wa fedha ndani ya miezi saba kuanzia Julai hadi Februali tumepokea wageni 4530 tunaona idadi inazidi kuimarika hata kwa Watalii wa ndani kwasiku wanaweza kupokelewa hadi wageni 200 "amesema Waziri Kairuki
Waziri ameendelea kwa kusema wanaendelea kuboresha miundombinu kama ujenzi wa gati za kisasa kuendelea kuandika maandiko maalumu na kushauriana na Wizara ya Uchukuzi ili waone ni gati gani imara na za kisasa zitakazo weza kupokea Meli kubwa za Utalii na za kisasa kama ilivyo onekana kwa mwezi Februali wamepokelewa wageni takribani 965.
"Tunaendelea lea kutangaza vivutio na mnaona njinsi gani kiwango hichi kinavyoendelea kuongezeka,Tunaendelea kujipanga kama wizara kuendelea kuvumbua maeneo mengi zaidi ya Utalii na Vivutio vyetu lakini pia kuyalinda maeneo yetu yasiweze kuharibiwa na kuhakikisha tunaendelea kuwa na ile hadhi ya Urithi wadunia.
Niendelee kuwakaribisha Watanzania wote kuweza kutembelea Kilwa Kisiwani maeneo ambayo Duniani watu wanatamani kuja kuyatembelea sisi tunayo tayari kwa Watalii wandani mnakaribishwa sana na gharama zake ni sakawaida sana,Tunawakaribisha kuwekeza katika miundombinu ya Malazi ,Chakula na hata maduka ya zawadi"amesema waziri Kairuki.
Naye Timotheo Mzava mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii amesema wamekuja kutembelea miradi na kugagua mradi wa kuboresha Hifadhi ya Malikale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara na wameridhishwa na utegelezwaji wa miradi hiyo.
"Kama kamati tumeridhika na kilicho fanyika ila tumetoa wito kwa wenzetu wa Mamlaka ya Wanyama Pori Tanzania (TAWA) na Wzara ya Maliasili kuongeza juhudi kubaini vivutio vya aina hii pia kuongeza juhudi kwenye kuongeza na kuboresha miundombinu ili kuongeza idadi ya Watalii na kuongeza mapato yatokanayo na shuguli za Utalii"
"Tumeona faida ya kuboresha miundombinu hii imesaidia kuongeza idadi ya watalii na kuongeza mapato kutoka Sh 18 Milioni hadi sh 65 Milioni kwa mwaka wa fedha wa 2022-23 yanayotokana na Utalii"amesema Mzava Mwenyekiti kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
0 Comments