Na Scolastica Msewa, Kibaha
MWENYEKITI wa Wazazi Mkoa wa Morogoro (CCM), Dk. Rose Rwakatare ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (PhD) na Chuo Kikuu cha All Nations Christian Church International University kilichopo Texas Marekani (ANCCI) kutokana na mchango wake kwenye jamii.
Hafla ya kutoa shahada hiyo kwa watu mbalimbali imefanyika leo Kibaha kwa Mbonde Mkoa wa Pwani ambapo mwakilishi wa chuo hicho ambaye ni raia wa Kenya, Profesa Purity Gatobu alitunuku Shahada hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa Sahahada hiyo, Dk. Rwakatare amesema kwa muda mrefu ametumia karama alizojaliwa na Mungu kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii wakiwemo wanawake, watoto na vijana kwa kuwapa nyenzo mbalimbali za kuwawezesha kuondokana na umaskini kama elimu ya ujasiriamali.
“Hii ni mara ya pili Sasa natunukiwa Udakaktari wa heshima na kwakuwa Mimi pia ni Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro nashukuru sana kwa chuo hiki kunitambua kwa kazi zangu na imenipa moyo kwamba kumbe dunia inaona kazi ninayofanya,” alisema
Dk. Rwakatare ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule za St Mary’s na East Africa, alisema Shahada aliyotunukiwa imempa ari ya kuendelea kutumikia jamii kwa kutoa msaada mbalimbali kwenye jamii.
Aidha kuelekea chaguzi za serikali za mitaa amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea Uongozi wa vitongoji na vijiji wakati utakapofika.
Amepongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa Uongozi uliotukukaka kwa Wananchi nchini.
Akizungumzia miaka mitatu ya utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amepongeza utekezaji Ilani ya CCM, kero za wananchi kutatuliwa sambamba na wananchi kusogezewa huduma za jamii ikiwemo sekta ya afya, elimu na huduma ya maji safi na salama.
0 Comments