Header Ads Widget

RC'S DC'S KUPATIWA FEDHA ZA USIMAMIZI SHUGHULI ZA KILIMO NCHINI

 


Na Hamida Ramadhani Matukio Daima app Dodoma


WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ya Kilimo itatoa shilingi milioni 10 kwa Kila Mkuu wa mkoa na shilingi milioni 5 kwa kila mkuu wa Wilaya lengo likiwa ni kuwafanya waweze kufuatatilia shughuli za Kilimo hapa nchini. 


Bashe ameyasema hayo leo jijini hapa kwenye mkutano wa wadau wa Tasnia ya Pamba kikao kilicholenga kutoa tathimini ya miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo sekta ya Pamba inaendelea kukua kutoka  kuzalisha Tani 174 , 486 Hadi kufikia 282510 kwa Mwaka 2022/2023.



Aidha amesema kuwa katika bajeti hiyo watagawa magari na kujenga nyumba kwa maafisa ugani ambapo kwa bajeti hiyo pia wataoa magari 50 kwa maafisa Kilimo mkoa na maafisa Kilimo wa wilaya . 


"Wizara inakwenda kujaza mafuta pikipiki za maafisa ugani lengo ni kuondoa malalamiko ya kutokwenda kwa wakulima mashambani kwa kigezo cha kukosa mafuta na kwa hatua hiyo sasa tupo kwenye usajili wa wakulima tu nataka kujua mpaka sasa tuna wakulima wangapi na tunawasaidiaje uzuri baadhi ya wakulima wanaendelea kufanya usajili, "amesema Waziri Bashe. 


Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini (TCB) Marco Mtunga amesema Uzalishaji wa pamba baada ya msimu wa bei 2019 /20 walizalisha 348.77 baada yakupata hapo uzalishaji ulishuka baada ya mwenendo wa bei na wakulima walivyoweza kipata shida wakati ule. 



Baada ya kushirikiana na maelekezo ya Waziri wameweza kufanya mabadiliko makubwa na uzalishaji umeweza kufikia tani 282000 msimu huu tunaoishia 


"Vita kubwa tunayoendelea nayo ni kwamba mazao mengi likiwemo zao la pamba tija iko chini ndio tunapambana kuweza kurekebisha hiyo kasoro ili uzalishaji wa pamba uweze kuongezeka na Pato la mkulima kuongezeka, "Mkurungenzi huyo .


Amesema kwa sasa iko hivi mkulima anayezalisha kilo 200 pato lake ni dogo ukilinganisha na mkulima anayezalisha kilo 1000.


"Chakwanza tunachokwenda kukifanya mkulima ana kwenda kupanda kwa vipimo ili kupata idadi ya miche sahihi inayotakiwa kwenye eneo na kuboresha huduma za ugani ili elimu kwa matumizi ya viwatilifu na upandaji na shughuli zote za Kilimo ziweze kusimamiwa kwa karibu zaidi, " Amesema. 


Na kuongeza "Tumeweza kusajili wakulima wawezeshaji zaidi ya 5000 ambao wapo karibu kila kijiji hao watatengeneza mtandao wa utoaji wa huduma za ugani kwamana badala ya afisa Kilimo mmoja kwenye kata watakuwa na watendaji wengine Saba hadi 10 ambao ni wakulima wanaozalisha vizuri nayo itasaidia Serikali kuajiri maafisa Kilimo wengi. 


Akiongelea suala la maafisa ugani kutofika kwa wakulima kwa kigezo cha pikipiki kukosa mafuta amesema ni kweli pikipiki zimesambazwa kila sehemu na wakurugenzi watendaji wametakiwa kusambaza mafuta ili maafisa ugani waweze kufanya kazi lakini Serikali imekuja na jambo jema kwa wakulima ambapo kwa Mwaka huu wafedha Serikali inakwenda kutenga fedha ya mafuta ya pikipiki kwa maafisa Kilimo kuweza kufanya kazi bila shida yoyote. 


Naye Mwenyekiti wa Bodi Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania Christopher Mwita Ghachuma, Amesema kwenye sekta ya Pamba kumekuwepo na matatizo mengi ambayo mengine wanayamudu kuyatatua na mengine yapo nje ya uwezo wao


"Tunaiomba serikali yetu sikivu zile changamoto tunazoshindwa kuzitatua hasa sisi wakulima wa Pamba itusaidie ili tuone tija ya ukulima wetu, "amesema Mwenyekiti Huyo


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI