Header Ads Widget

BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

 

NA THABIT MADAI,ZANZIBAR- MATUKIO DAIMA

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imesema kwamba, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uboreshwaji wa miondombinu ya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume unatokelezwa kwa Fedha za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bilioni 70.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi ya Viwanja vya Ndege, Lela Burhan Ngozi wakati wa ziara maalum ya kutembelea na kukagua utekelezaji  wa Miradi ya Maendeleo ya  katika Uwanja vya Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume.


Amesema kwamba,  hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo inaridhisha kwa asilimia kubwa  licha ya kuanza kwa muda mfupi utekelezaji  wake.

"Tumekuja hapa kuangalia utekelezaji wa miradi katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Abeid Karume  ambapo tumeridhishwa kwa Asilimia zote kutokana miradi hii imeanza kwa muda mfupi sana," amesema.

Ameongeza kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo itaisaidia kuongeza huduma bora katika Viwanja vya Ndege na kuchochea Uchumi wa Nchi.

Aidha amesema kuwa, utekelezaji wa Miradi hiyo inakwenda sambamba  na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

" Kwa Kweli Rais Dk. Mwinyi amefanikiwa kutekeleza kwa asilimia zaidi ya 100 ilani ya chamade Mapinduzi  ambapo amefanikiwa kuvuka lengo lililowekwa," ameeleza.


Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Kanali  Amour Jeni amesema kwamba, lengo la ziara hiyo ni kuangalia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kufuatia maagizo ya Serikali.

"Serikali chini ya Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa maagizo ambayo leo tumekuja kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi lengo kuimarisha na kuboresha miondombinu ya Viwanja vyetu vya ndege," ameeleza.

Mapema,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Seif Abdallah Juma amesema kuwa, utekelezaji wa Miradi unakwenda kuimarisha utoaji wa Huduma ndani ya Viwanja vya ndege na kuongeza ushindano ndani na Nje  ya Afrika.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS