Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, amefanya ziara ya kukagua miradi mitatu ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmshauri ya Manispaa ya Lindi yenye thamani ya Bilioni 15.7 .
Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati uliopangwa, Mhe. Telack amekagua Mradi wa Ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Lindi wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.8 unaolenga kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara. Ambapo katika mradi huo hali ya utekelezaji bado ipo chini.
Katika Mradi wa Ujenzi wa stendi kuu ya mabasi unaojengwa Mtaa wa Mitwero Manispaa ya Lindi unaogharimu Tsh. Bilioni 7.8 ambao unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri na kuchochea shughuli za uchumi katika manispaa na Mkoa kwa ujumla , Mhe Telack ametoa maelekezo kwa mkandarasi yakumtaka kuongeza kasi, kuzingatia ubora, kuongeza idadi ya wafanyakazi na kuweka taa eneo hilo ili kazi ziweze kufanyika usiku na mchana.
“Fungeni taa, hela ya serikali mnayo, yani mimi nikija hapa leo saa mbili usiku nikute watu wanafanya kazi , na nikute mixer zile ziko zaidi ya moja , nikute watu hapa wanafanya kazi hadi kesho asubuhi “ Mhe. RC Telack.
Awali katika ujenzi huo , amemtaka mshauri wa mradi kuhakikisha ubora na viwango vinazingatiwa na kuwepo eneo la ujenzi muda wote.
Kwa upande wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Lindi zilizopo Mtaa wa Mitema wenye thamani ya Tsh. Bilioni 4, Mhe Telack ameagiza kuhakikisha ndani ya wiki mbili hatua ya msingi ya awali iwe imekamilika kama ambavyo wamekubaliana na mkandarasi .
Aidha, Mhe Telack, amemtaka mkandarasi ambaye ni Hamerwork Internatinali Limited kwa kushirikiana na KIMKIM Contractors Limited, kuhakikisha ujenzi unatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na kukamilika kwa wakati uliopangwa ili kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.








0 Comments