Header Ads Widget

ACT: MCHAKATO KUPATA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI UANZE SASA

 


Makamu Mwenyekiti ACT-WAZALENDO (Bara), Isihaka Mchinjita. Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam.

NA MATUKIO DAIMA APP, DAR

CHAMA  cha ACT Wazalendo, kupitia kwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Isihaka Mchinjita, kimewataka wajumbe wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wajiuzulu ili kupisha mchakato wa kuundwa kwa Tume mpya ya Uchaguzi uanze kwa mujibu wa Sheria.


Sheria hiyo  ya Tume ya Uchaguzi ilipitishwa na Bunge hivi karibuni. 


Akizingumza leo Machi 24 2024, Mchinjita amesema Tume hiyo mpya itapatikana kwa ushindani wa Watanzania kuomba, kusailiwa na Jopo Maalumu, kuchujwa na kisha kuteuliwa; 


"Tunataka Tume hiyo moya iratibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwishoni mwa mwaka huu 2024, na pia

iendeshe Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025" amesema Mchinjita na kuongeza kuwa


Kwa heshima na taadhima, makamishna wa NEC waliopo wanapaswa kuwapa nafasi Watanzania kupata NEC mpya kwa mujibu wa Sheria mpya ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 

Makamu huyo Mwenyekiti chama hicho amesema kuwa busara inataka Makamishna hao wote wajiuzulu kwa mpigo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS