IMEELEZWA kuwa ongezeko
la vijana wenye mazingira magumu
katika jamii imesababishwa na baadhi ya
wazazi na walezi ambao
kipato chao cha
chini hivyo kushindwa
kuwalea vema vijana
wao kutokana na fikra
mgando waliziokuwa nazo za kuishi Maisha ya kimasini wakati vijana hao
wanao uwezo mkubwa wa kuzipambania familia
zao kuwa na Uchumi bora kutokana na raslimali ardhi walionayo vijijini .
Kuwa ukifuatilia
chimbuko la vijana wenye mazingira magumu unakuta linatoka ndani ya
familia na sababu kubwa ni familia kukata tamaa na kuona
kujimilikisha mzigo wa umasikini kama ni
haki ya familia kuishi Maisha ya kimasikini
pamoja na kuwa na ardhi nzuri kwa kilimo
jambo ambalo si sawa
.
Kwani kwa
kawaida ardhi ni mtaji mkubwa
kuliko mali nyingine yoyote
na ukiwa na ardhi unauwezo wa
kufanya maendeleo makubwa nay a haraka zaidi
kupitia ardhi tofauti na ukiwa na pesa pasipo ardhi
.
“Tambua pes ani kila kitu japo ardhi ni zaidi ya pesa maana hata mwenye pesa ni lazima kumtafuta mwenye ardhi ili afanya shughuli za kilimo ama uwekezaji hivyo unaweza kuwa na pesa nyingi ila ni lazima ukatafuta mtu mwenye ardhi kama ardhi ni mtaji hakuna sababu ya vijana wanaotokana na familia za wazazi wenye ardhi nao kuishi Maisha ya umasikini hasa katika nyakati hizi ambazo thamani ya ardhi ni kubwa zaidi “
Halfayo Mwalongo mwanafunzi
wa mchepuo wa
ujasiriamali na vitendo na mkufunzi wa mafunzo ya
ujasiriamali na vitendo kutoka chuo
kikuu cha Iringa
aliyasema hayo leo katika
ukumbi wa Yatima
wakati wa warsha
ya kuwajengea uwezo
wa kiuchumi vijana 140 kutoka
vijiji vya kata tatu
za Mdabulo ,Ihanu na Luhunga katika
wilaya ya Mufindi mkoa
wa Iringa chini ya ufadhili wa
mradi wa Youth Angecy Mufindi ( YAM).
Alisema vijana hao
wanatoka ndani ya vijiji
zaidi ya 15 vya
kata hizo tatu
hivyo kupitia mafunzo
hayo watakwenda kuwa
chachu ya vijana
na familia nyingine
kutokata tamaa ya
Maisha kutokana na hali
duni ya kiuchumi .
Mwalongo alisema wilaya
ya Mufindi ni wilaya
yenye Uchumi mzuri
ukilinganisha na baadhi ya
wilaya hapa nchini kwani
mazao ya biashara yanayostawi katika
ardhi ya wilaya ya Mufindi ni fursa pekee kwa
wananchi kuondokana na changamoto ya
kiuchumi iwapo wataitumia vizuri
fursa hiyo.
Hata hivyo alisema
kwa vijana hao wa
mradi wa YAM ambao wengi wao walionesha kukata
tamaa ya Maisha kutokana na
hali duni ya kimaisha katika
familia zao baada ya mafunzo hayo watakwenda
kuwa tofauti na vijana
wenzao ambao hawajafikiwa na mradi huo kwani mafunzo hayo yatawafungua Kwenda kuchangamkia
fursa ardhi inayowazunguka .
Alisema kuwa vijana
wengi wamekuwa wakikata
tamaa ya kimaisha kutokana na ugumu wa Maisha kwa
kuhisi kukosa mtaji fedha
wa kuendesha Maisha japo
wamesahau kuwa pesa
sio mtaji pekee bali ardhi
ni mtaji wa uhakika katika Maisha .
Hivyo alisema kutokana na mafunzo hayo wataweza kutambua
fursa zinazowazunguka na
jinsi ya kuzitumia fursa
zinazopatikana katika maeneo yao kuelekea
katika mafanikio ya
kiuchumi pia kuondokana na
fikra mgando na
kuwa na fikra Chanya za
kuwawezesha Kwenda kujitegemea
wenyewe .
“ Mafunzo haya
yamewapa uwezo wa kutambua
fursa kubwa zinazowazunguka ambazo mara ya
kwanza hawakuweza kuzitambua
kwani wamepewa uwezo
wa kutambua mitaji yao na
jinsi ya kuipata kutokana na mazingira yanayowazunguka na kupitia
mafunzo hayo watakwenda kuwa
chachu katika familia zao”
Mwalongo alisema
kuwa mradi huo wa
YAM umekuwa msaada mkubwa kwa
vijana hao ambao
siku zote walikuwa wakilala
na kuamka kwenye fursa huku
Maisha yao yakiendelea
kuwa duni pamoja na kuishi familia
ya fursa .
Hivyo alitaka jamii kuepuka
kuwakatisha tamaa ya Maisha vijana
kwa kigezo cha umasikini
wa wazazi wao kwani
umasikini ni ugonjwa unaoambukizwa ambao unaweza kuikumba familia nzima na
sio lazima kuzaliwa familia
masikini ni sababu ya kila mmoja
kuwa masikini kwenye familia kwa
kutumia fursa zilizopo za ardhi unaweza
kuzaliwa kwenye familia
masikini ila wewe ukawa tajiri mkubwa .
Edina Mwagala
mkazi wa Kijiji cha Ikanga
kata ya Mdabulo ni mmoja
wa wanufaika wa
mafunzo hayo alisema wakati anachaguliwa
kuingia katika mafunzo hayo ya
bure hakutambua kama atakuwa na upeo mkubwa
wa kufikiri kuwa na ndoto ya
kuanza safari ya kujikwamua
kiuchumi kupitia fursa zinazomzunguka .
0 Comments