Header Ads Widget

ACT YAONYA FAULO UCHAGUZI WA DIWANI KIGOMA UJIJI

 


Katibu wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma Yunus Luhonvya (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Kasingirima Ahamd Alumbula  (kulia)  kwenye mkutano wa hadhara eneo la Madrasat Nur kutafuta kura za mgombea wa ACT kwenye uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Kasingirima Kigoma Ujiji


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kuwa hakitakubali kuona hila zinatumika kumtangaza mshindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kasingirima Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo wametaka mshindi halali wa uchaguzi huo ataangazwe.

 

Mwenyekiti wa ngome ya ngome ya vijana Taifa ACT,Abdul Nondo alisema hayo katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa chama hicho ambapo alisema kuwa chama hicho kinataka demokrasia itumike katika kumpata mshindi.

 

Nondo alisema kuwa wameingia kwenye uchaguzi huo kutimiza malengo ya demokrasia katika kuwapatia wananchi muwakilishi wao hivyo ametaka maamuzi ya wananchi katika kumpata mshindi yaheshimiwe badaalaa ya hila na wizi kutumika kumpata mshindi.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni Katibu wa ACT mkoa Kigoma,Yunus Luhonvya alisema kuwa wamejizatiti kuhakikisha mgombea wao anakuwa chaguo la wapiga kura ili uchaguzi uwe wa haki na amani.

 

Hata hivyo Luhonvya alisema kuwa hawatakubali kuona yale yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 yanatokea kwenye uchaguzi huo mdogo na kuwaonya wasimamizi wa uchaguzi huo kusimamia uchaguzi kwa haki na kuhakikisha haki inatendeka ili amani itawale kwenye uchaguzi huo.

 


Kwa upande wake mgombea wa ACT Wazalendo katika uchaguzi huo mdogo wa udiwani wa kata ya Kasingirima Manispaa ya Kigoma Ujiji, Ahamad Alumbula aliomba wananchi wampigie kura za ndiyo ili awatumikie na kuahidi kutekeleza yale yote ambayo ameahidi ikiwemo ujenzi wa choo katika soko la Kwa Noti Ujiji ambapo kwenye mkutano huo ahadi ya mifuko 40 ya sement ilitolewa, tofali 1500 huku yeye akieleza kuwa na tofali zote kwa ajili ya choo hicho.


uchaguzi mdogo wa kata ya Kasingirima unatarajia kufanyika Machi 20 mwaka huu kuziba nafasi ya aliyelkuwa diwani wa kata hiyo Abdallah Kiembe ambaye amepata ajira serikali

 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI